// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKE WA MAREHEMU SAHAU KAMBI, REHEMA TAJIRI ARUDI KWA KISHINDO KWENYE MUZIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKE WA MAREHEMU SAHAU KAMBI, REHEMA TAJIRI ARUDI KWA KISHINDO KWENYE MUZIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 06, 2014

    MKE WA MAREHEMU SAHAU KAMBI, REHEMA TAJIRI ARUDI KWA KISHINDO KWENYE MUZIKI

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    MKE wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Sahau Said Kambi (sasa marehemu), Rehema Tajiri amerejea kwa kishindo kwenye anga za muziki kwa kuipua nyimbo mpya, ambazo ameziita kali.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, mke huyo wa kipa wa zamani wa Yanga SC, alisema kwamba safari hii amepania kuliteka kweli soko la muziki Tanzania. 
    Nimerudi kwa hasira; Rehema Tajiri amerejea kwenye anga la muziki baada ya kimya cha muda mrefu kwa kutoa nyimbo mpya kali 

    Alisema wimbo wa kwanza unaitwa Raha Leo ambao umepigwa katika mtindo wa mduara akimshirikisha Abdully na kurekodiwa katika studio za Tanzania House Of Talent (T.H.T.) chini ya prodyuza Imma The Boy. 
    Wimbo mwingine ni Yote Maisha uliorekodiwa katika studio za Smart zilizopo Tabata akimshirikisha gwiji wa Bongo Fleva, Inspekta Haroun ‘Babu’. 
    “Nyimbo nyingine mbili bado zipo studio na hazijapewa majina, nilikuwa kimya tangu msiba wa marehemu mume wangu, ila sasa nimeamua kurudi. Safari hii nakuja kikazi sana tofauti na kipindi cha nyuma,”alisema Rehema. 
    Rehema amesema sasa yuko tayari kufanya maonyesho katika kumbi mbalimbali na anapokea mialiko moja kwa moja kupitia namba yake (0713 412624).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKE WA MAREHEMU SAHAU KAMBI, REHEMA TAJIRI ARUDI KWA KISHINDO KWENYE MUZIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top