KOCHA David Moyes jana alilazimika kufanya na mazoezi na wachezaji katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki.
Manchester United leo inahitaji kukipiku kipigo cha mabao 2-0 ilichokipata kutoka kwa wapinzani wao hao katika mchezo wa kwanza ugenini- maana yake ishinde 3-0 ndio isonge Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa.
Wachezaji wa United jana walionekana wenye nia ya kufanya kile ambacho wengi hawatarajii leo Uwanja wa Old Trafford watakapokutana na Olympiacos.
England imefanikiwa kuingiza timu moja tu Robo Fainali hadi sasa, ambayo ni Chelsea iliyoitoa Galatasaray jana kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya Manchester City na Arsenal kutolewa na timu zilizokutana kwenye fainali ya mwaka jana, Bayern Munich waliotwaa ubingwa na Barcelona waliovuliwa taji.
Hakika United wanakabiliwa na mtihani mgumu, kushinda mabao 3-0 nyumbani dhidi ya timu inayoonekana kuwa imara, lakini wamedhamiria kupigania hilo.

Anajifua nao: Moyes alijumuika na wachezaji wake mazoezini jana kwa maandalizi ya mechi na Olympiacos
Wote pamoja sasa? United wameunganisha nguvu zao kuhakikisha wanaitoa Olympiacos
"Nafikiri sapoti ndani ya Old Trafford imekuwa babu kubwa,"alisema jana Moyes.
"Nimewaambia wachezaji tunahitaji kurejesha makali yetu sasa, tunahitaji kuanza kucheza pamoja. Mimi na timu. Tunahitaji kuhakikisha kwamba tunapambana pamoja kucheza vizuri katika usiku ambao utakuwa wa kukumbukwa.
"Wote hakuna tulichoacha nyuma kuelekea usiku huo, ni matumaini tutajaribu kuhakikisha kwamba tunasonga mbele,"alisema Moyes.
0 comments:
Post a Comment