KOCHA Manuel Pellegrini anaamini Manchester City wanaweza kushinda michezo yote 11 zilizobaki na kubeba taji la Ligi Kuu ya England - lakini watalazimika kucheza bila mfungaji wao bora Sergio Aguero katika mechi zisizopungua mbili.
Mshambuliaji huyo wa Argentina, ambaye alfunga bao lililoipa ubingwa City katika mechi ya mwisho msimu wa 2012, atakuwa nje kuanzia mechi ya leo dhidi ya Fulham na Jumanne dhidi ya wapinzani, Manchester United kutokana na maumivu ya ya nyama za paja.
Pellegrini anatarajia Aguero kufanya mazoezi wiki ijayo,lakini pia anaweza kukosa pia mechi dhidi Arsenal wikiendi ijayo.
Majeruhi: Aguero ameumia na atakuwa nje katika mechi mbili ikiwemo ya Jumanne dhidi ya Manchester United
Alipoumia: Aguero alipata maumivu wakati City ikitolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Barcelona
"Sina uhakika kuhusu Arsenal," alisema kocha huyo City. "Tutaona atakaporejea, lakini hana nafasi kabisa katika mechi United. "Labda wiki ijayo ataanza kufanya kazi na wenzake,lakini sifikiri kwa wiki yote,".
City inaachwa na vinara Chelsea kwa pointi sita, lakini bado wana nafasi ya ubingwa kutokana na kuwa na mechi tatu mkononi, na Pellegrini anaamini wachezaji wake wanaweza kuendeleza wimbi la ushindi hadi mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment