// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI AWAPA NENO SIMBA SC KUELEKEA MKUTANO WAO JUMAPILI, AWAKUMBUSHA WARAKA WA TFF WALIOTUMIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI AWAPA NENO SIMBA SC KUELEKEA MKUTANO WAO JUMAPILI, AWAKUMBUSHA WARAKA WA TFF WALIOTUMIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 14, 2014

    MALINZI AWAPA NENO SIMBA SC KUELEKEA MKUTANO WAO JUMAPILI, AWAKUMBUSHA WARAKA WA TFF WALIOTUMIWA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    RAIS Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la heri Simba SC katika mkutano wa wanachama wake utakaofanyika Jumapili (Machi 16 mwaka huu) kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
    “Nachukua fursa hii kuwatakia kila la heri katika mkutano huo ambao ni muhimu katika kuhakikisha klabu yao inapiga hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu na ustawi wake kwa ujumla,”amesema Malinzi.
    Jamal Malinzi kushoto akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kulia

    Hata hivyo, Malinzi amewakumbusha viongozi na wanachama wa klabu ya Simba kuwa marekebisho hayo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na maelekezo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Afrika (CAF) na Tanzania (TFF).
    Amewataka kuuzingatia waraka wa TFF kwa wanachama wake wa Februari 7 mwaka huu katika marekebisho hayo.
    “TFF inawatakia wanachama wa Simba mkutano mwema, na inawakumbusha wazingatie umuhimu wa kudumisha amani na maelewano katika klabu yao,”amesema.
    Wakati huo huo: Semina ya siku mbili kwa waamuzi wenye beji za FIFA na wale wa ngazi ya juu nchini (elite) kwa robo ya kwanza ya mwaka huu inaanza kesho (Machi 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Waamuzi na waamuzi wasaidizi 22 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika semina hiyo ambayo pia itahusisha mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test), na itamalizika keshokutwa (Machi 16 mwaka huu).  
    Baadhi ya waamuzi hao ni Charles Simon kutoka Dodoma, Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa) na Jesse Erasmo (Morogoro).
    John Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa (Bukoba), Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Ramadhan Ibada (Zanzibar) na Waziri Sheha (Zanzibar).
    Katika hatua nyingine, Watanzania watano wameteuliwa kuingia kwenye jopo la makamishna watakaosimamia mechi mbalimbali za CAF kwa mwaka 2014 hadi 2016.
    Kwa mujibu wa orodha iliyotumwa na CAF kwa TFF, Watanzania hao ni Alfred Kishongole Rwiza wa Mwanza na Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar ambao wamerejeshwa tena kwenye jopo hilo.
    Rwiza na Tahir ambao ni waamuzi wastaafu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wakufunzi wa uamuzi walikuwepo kwenye jopo lililopita la 2012 hadi 2014.
    Makamishna wapya kwa upande wa wanawake ni Elizabeth Mwanguku Kalinga wa Mbeya na Isabellah Hussein Kapera wa Dar es Salaam. Kamishna mwingine mpya kwa upande wa wanaume ni Muhsin Ali Rajab kutoka Zanzibar.
    Wakati huo huo, CAF imeandaa semina kwa makamishna wanaume itakayofanyika jijini Cairo, Misri kuanzia Aprili 3 hadi 4 mwaka huu.
    Watoa mada kwenye semina hiyo ya siku mbili ni Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani, Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Shereen Arafa na Naibu Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Khaled Nassar.
    Wengine ni Meneja wa Waamuzi wa CAF, Eddy Maillet, Mkurugenzi wa Habari wa CAF, Junior Binyam, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano wa CAF, Tarek el Deeb na Mkurugenzi wa Masoko na Televisheni wa CAF, Amr Shaheen.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAPA NENO SIMBA SC KUELEKEA MKUTANO WAO JUMAPILI, AWAKUMBUSHA WARAKA WA TFF WALIOTUMIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top