Na Dina Ismail, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa, Fadhili ‘Tiger’Awadh amefariki dunia katika hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni, Dar es salaam jana baada ya kuugua kwa siku kadhaa ugonwa wa Malaria.
Fadhili Awadh amefariki akiwa tayari amesaini Mkataba wa kupanda ulingoni kwa ajili ya pambano la ubingwa Machi 29, mwaka huu kuzipiga na Alan Kamote wa Tanga na tayari alikuwa kwenye maandalizi ya mpambano huo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daktari, sababu ya kifo chake ni ugonjwa wa Malaria ambao alijaribu kuutibu kwa dawa aina ya Metakelfin, lakini hali yake ilibadilika akiwa mazoezini na kuanza kujisikia vibaya, hivyo kuwahishwa katika hospitali hiyo ambako baada ya siku mbili alifariki dunia jana akiwa na umri wa maika 32.
Bondia huyo alikuwa ana maendeleo mazuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kupewa pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam akiwasindikiza Japhet Kaseba na Thomas Mashali.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Manzese, Dar es Salaam ambako taratibu za maizishi zinaendelea.
Pumzika kwa amani Fadhili Awadh ‘Tiger’.

Pimzika kwa amani; Bondia Fadhil 'Tiger' Awadh enzi za uhai wake |
Kwa mujibu wa taarifa ya Daktari, sababu ya kifo chake ni ugonjwa wa Malaria ambao alijaribu kuutibu kwa dawa aina ya Metakelfin, lakini hali yake ilibadilika akiwa mazoezini na kuanza kujisikia vibaya, hivyo kuwahishwa katika hospitali hiyo ambako baada ya siku mbili alifariki dunia jana akiwa na umri wa maika 32.
Bondia huyo alikuwa ana maendeleo mazuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kupewa pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam akiwasindikiza Japhet Kaseba na Thomas Mashali.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Manzese, Dar es Salaam ambako taratibu za maizishi zinaendelea.
Pumzika kwa amani Fadhili Awadh ‘Tiger’.
0 comments:
Post a Comment