MWANASOKA bora wa dunia, Christiano Ronaldo alimkasirikia Gareth Bale jana wakati Real Madrid ikifungwa kwa mara ya pili ndani ya siku nne katika La Liga na kupigwa kumbo na Barcelona na Atletico Madrid katika mbio za ubingwa.
Huku Real ikichapwa mabao 2-1 na Sevilla, Ronaldo alishindwa kuficha hasira zake baada ya mwanasoka ghali duniani, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86, Bale alipoamua kupiga mpira wa adhabu, badala ya kumuachia mshambuliaji huyo Mreno, na akaenda kupiga juu ya lango.
Ronaldo lionyeshwa na kamera za TV akimuwakia Bale baada ya kupiga ovyo faulo hiyo.
Unatuzingua mwana: Cristiano Ronaldo akimuwakia Gareth Bale baada ya nyota huyo wa Wales kupiga ovyo faulo
Nani, mimi? Bale aliwakiwa na Ronaldo aliyepagawa na kipigo cha pili Real Madrid
Ilikuwa ni siku mbaya kwa mwanasoka huyo wa Wales, ambaye alitoka uwanjani mara moja kwenda kubadilisha viatu na kuiacha Real ikiwa pungufu na wachezaji 10. Wakati anabadilisha viatu, Carlos Bacca ndipo alipoifungia bao la ushindi Sevilla dakika ya 73.
Kipigo cha Madrid Uwanja wa Sanchez Pizjuan jana, kinakuja siku nne baada ya kufungwa na Barcelona, Lionel Messi akimfunika Ronaldo kwa kufunga hat trick katika ushindi wa 4-3 mjini Madrid.
MATOKEO YA MECHI ZA JANA LA LIGA
Vipigo hivyo mfululizo,vinakuja baada ya timu ya Carlo Ancelotti kucheza mechi 31 mfululizo bila kupoteza hata moja.
"Tunatakiwa kuendelea kufanya kazi, kupambana na kuwaomba msamaha mashabiki wetu,"alisema beki wa pembeni wa Madrid, Marcelo.
Hana furaha: Ronaldo alishindwa kuficha hisia zake wakati Real Madrid ikifungwa na Sevilla
Mshambuliaji huyo wa Columbia alitua Sevilla kwa Pauni Milioni 6 msimu huu na sasa amekwishafunga mabao 18 kwenye mashindano yote msimu huu.
Alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kipindi cha kwanza pia kufunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa pasi ya Jose Antonio Reyes na kipindi cha pili alifunga kwa pasi ya Ivan Rakitich, kiungo wa Croatia aliyemtoka vizuri Pepe na kumpasia Bacca aliyemtungua kipa Diego Lopez kukamilisha ushindi wa 2-1. Ronaldo alifunga bao la Real dakika ya 14.
Huku Atletico Madrid ikiifunga Granada 1-0, bao pekee la Diego Costa dakika ya 63, nayo Barcelona iliitandika 3-0 Celta mabao ya Neymar dakika ya sita na 67 na Messi dakika 30.
Matokeo hayo, yanaifanya Atletico inayofundishwa na kocha Diego Simeone ipae kileleni mwa Liga kwa kufikisha pointi 73, Barcelona iliyofikisha pointi 72 sasa ya pili na Real inayobaki na pointi zake 70 inakuwa ya tatu.
Soka, au mapigano; Ronaldo akipambana na mchezaji wa Sevilla, Stephane M'Bia
La ushindi: Bacca akimtungua kipawa Real Diego Lopez, kuifungia bao la ushindi timu yake
Ndiyo maana yake: Kondakta wa basi wa zamani akishangilia baada ya kuiua Real jana
Mabao: Mabao mawili ya Neymar na moja la Lionel Messi yameirejesha rasmi Barcelona kwenye mbio za ubingwa
Mkali hatari: Diego Costa ameifungia bao la ushindi Atletico Madrid dhidi ya Granada
0 comments:
Post a Comment