KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba refa Chris Foy anastahili lawama kwa rafu ambayo Ramires alimchezea Karim el Ahmadi.
Ramires alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Foy katika sekunde za mwishoni Chelsea ikifungwa 1-0 na Aston Villa Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na atakosa mechi dhidi ya Arsenal, Crystal Palace na Stoke za ligi hiyo akitumikia adhabu yake.
Mourinho hakufurahishwa na kiungo wake Mbrazil kwa kuonyesha utovu wa nidhamu, lakini amesistiza marefa lazima wabebe majukumu ya kuwatuliza wachezaji uwanjani.
Timba timba: Ramires akimtimba Karim el Ahmadi Uwanja wa Villa Park Jumamosi,rafu ambayo ilimponza alimwe kadi nyekundu
Kwenda nje: Refa Chris Foy akimuonyesha kadi nyekundu Ramires
Mgogoro wa mwisho: Mourinho akimalizia hasira zake kwa refa wa akiba, Jon Moss, ambaye anamuonyesha njia ya kuelekea jukwaani
"Nimechukizwa na Ramires, lakini unafahamu, kwenye soka, ni vigumu kudhibiti hasira,"alisema Mourinho.
"Kuna watu ambao kwenye mchezoni jukumu lao kuwasaidia wachezaji kudhibiti hasira zao na wakati mwingine watu hao ndio wana sababisha wachezaji wapandishe jazba.
"Siwezi kutenganisha rafu ya Ramires — ambayo ilistahili kadi nyekundu — ilitokana na kupandwa na jazba wakati wa mchezo," aliongeza Mourinho ambaye naye pia siku hiyo alionyeshwa kadi nyekundu na mchezaji wake mwingine, Willian.
Kipigo cha Jumamosi kinaipunguza kasi Chelsea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England, sasa ikibani na pointi 66 baada ya kucheza mechi 30, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 62 za mechi 29, Arsenal pointi 62 mechi 29 na Manchester City pointi 60 mechi 27.
MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU ENGLAND ZILIVYOSHIKA KASI...
As it stands: The Premier League top four
0 comments:
Post a Comment