Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani Afrika, Enyimba ya Nigeria na Raja Club Athletic ya Morocco wametolewa kwenye Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana.
Wawili hao, ambao kwa pamoja wameshinda mataji matano ya michuano hiyo watakosa Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu Afrika baada ya matokeo mabaya jana mbele ya wapinzani wao.
Vigogo wa Nigeria, Enyimba walishinda bao 1-0 tu dhidi ya AS Real ya Mali mjini Bamako, shukrani kwake Bala Zaka aliyefunga, lakini halikutosha kuwasongesha mbele kutokana na kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani.
Timu ya Mali inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2.
Mjini Casablanca, mabingwa wa Guinea, Horoya, pia wamewatoa wababe wa michuano hiyo miaka ya 1970 na 1980, Raja. Mshambuliaji Mouhcine alifunga bao pekee kwenye mchezo huo dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho na kulazimisha mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti na Horoya ikashinda kwa 5-4.
Katika mechi za juzi, Zamalek ya Misri ilipenya kwenye tundu la sindano kuelekea Hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kulazimisha sare ya bila kufungana Angola mbele ya wenyeji Kabuscorp katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza.
Zamalek inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Misri na Tottenham Hotspur ya England na klabu hiyo ya Cairo, Ahmed Hassan ‘Mido’ ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani na kutengeneza hofu ya kutolewa.
Katika mechi za jana, KCC ya Uganda iliaga kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-3, ikifungwa 2-1 leo Kampala na Nkana FC ya Zambia baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza.
ASFA Yennenga ya Burkina Faso imeaga kwa kipigo cha jumla cha 5-0 kwa ES Setif ya Algeria baada ya sare ya 0-0 leo nyumbani, ikitoka kufungwa 5-0 Algiers wiki iliyopita na Primeiro de Agosto ya Angola imeaga kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-3 ikishinda 2-0 leo nyumbani baada ya kufungwa 4-1 na AC Leopards ya Kongo katika mchezo wa kwanza Brazzavile.
Liga Muculmana ya Msumbiji imetolewa pia kwa jumla ya mabao 7-0 na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini leo ikifungwa 3-0 nyumbani baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza.
Michuano hiyo inaendelea leo, mabingwa watetezi Al-Ahly ya Misri wakijaribu kukipiku kipigo cha 1-0 kutoka Yanga SC ya Tanzania, Ahli Benghazi ya Libya ikiikaribisha Berekum Chelsea ya Ghana baada ya sare ya 1-1 ugenini, Coton Sport ya Cameroon ikiikaribisha Flambeau de l’Est ya Burundi baada ya ushindi wa 1-0 Bujumbura, TP Mazembe ya DRC ikiikaribisha Astres Douala ya Cameroon baada ya sare ya 1-1 Douala, Sewe Sport ya Ivory Coast ikiikaribisha Barack Young Controllers ya Liberia baada ya sare ya 3-3 Monrovia.
CS Sfaxien ya Tunisia itakuwa mwenyeji wa Dedebit ya Ethiopia baada ya ushindi wa 2-1 Addis Ababa,
El Hilal Sudan itaikaribisha Stade Malien baada ya sare ya bila kufungana Mali na AS Vita Club ya DRC itaikaribisha Dynamos ya Zimbabwe baada ya sare ya bila kufungana Harare.

Wababe wa zamani; Enyimba wametolewa Ligi ya Mabingwa ya Afrika |

0 comments:
Post a Comment