AC MILAN imeungana na Arsenal kuipa mkono wa kwaheri michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutandikwa mabao 4-1 na Atletico Madrid usiku huu Uwanja wa Vicente Calderon katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora.
Milan sasa inaaga kwa kipigo cha jumla cha 5-1, baada ya awali kufungwa 1-0 nyumbani. Diego Costa alitangulia kuifungia Atletico dakika ya tatu pasi ya Koke, kabla ya Ricardo Kaka kuisawazishia Milan dakika ya 27 pasi ya Poli.
Milan ikatepeta na kuongezwa mabao matatu wafungaji Turan dakika ya 40, pasi ya Raul Garcia, aliyefunga la tatu dakika ya 71 kwa pasi ya Gabi na Diego Costa akakamilisha safari ya Atletico kuelekea Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa kwa bao zuri dakika ya 85 pasi ya Sosa.
0 comments:
Post a Comment