// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAF YAIPA TAIFA STARS MCHONGO WA JEZI ZA ADIDAS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAF YAIPA TAIFA STARS MCHONGO WA JEZI ZA ADIDAS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 09, 2014

    CAF YAIPA TAIFA STARS MCHONGO WA JEZI ZA ADIDAS

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kwamba kufuatia makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars), zikiwemo jezi ambazo zilianza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
    Uzi wenyewe ni huu; Jezi mpya za Adidas za Taifa Stars ambazo imepata kwa msaada wa CAF
    Amesema vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
    “TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,”amesema Malinzi.
    Mwezi uliopita, Malinzi alikwenda makao makuu ya CAF, Cairo nchini Misri kujitambulisha baada ya kurithi kiti cha Leodegar Tenga Desemba mwaka jana na akiwa huko alikutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou aliyeahidi kumpa sapoti kubwa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAIPA TAIFA STARS MCHONGO WA JEZI ZA ADIDAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top