MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wanaweza kuadhibiwa na UEFA baada ya kikundi cha mashabiki wake kupeperusha bango la udhalilishaji kwa wapinzani wao, Arsenal wakati wa mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Allianza Arena, tkimu hizo zikitoka sare ya 1-1.
Kwa matokeo hayo,Bayern wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 Uwanja wa Emirates mjini London.
Bango hilo lilikuwa linasomeka 'Gay Gunners' yaani Mashoga Gunners na lilionekana kumlenga kiungo Mesut Ozil likipeperushwa kabla ya mechi kuanza Uwanja wa Allianz Arena.
Licha ya kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kocha Joachim Low wa timu ya taifa ya Ujerumani, kiwango cha uchezaji cha Ozil siku za karibuni katika kikosi cha Arsene Wenger kinatiliwa shaka na mashabiki wake nchini mwake na vyombo vya habari vinautazama kwa jicho la tatu uwezekano wa kupata nafasi katika kikosi kitakachokwenda Brazil kwenye Kombe la Dunia.
0 comments:
Post a Comment