KOCHA Arsene Wenger leo amekabidhiwa tuzo ya dhahabu kwa kufikisha mechi 1,000 akiwa kazini Arsenal.
Mfaransa huyo atafikisha mechi ya 1,000 kesho atakaposafiri na The Gunners hadi Stamford Bridge kumenyana na Chelsea katika Ligi Kuu ya England mchana.
Kuheshimu hilo, Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick amemkabidhi Wenger tuzo hiyo leo asubuhi katika viwanja vya mazoezi ya klabu mbele ya Waandishi wa Habari.
Washika Bunduki: Wenger akiwa na Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kushoto) na Mwenyekiti Sir Chips Keswick (kulia) baada ya kupokea tuzo yake
Akizingatia wa timu kufanya vizuri na kufanya vibaya akiwa kazini, Wenger aliyeipa timu hiyo mataji matatu ya Ligi Kuu ya England na manne ya Kombe la FA, alisema; "Kila kipigo unachopata ni maumivu moyoni ambayo huwezi kusahau, na kila ushindi ni wa kusahau kwa sababu unachukuliwa ni kawaida,".
Aliongeza; "Kumekuwa na msoto mkubwa katika mechi 1,000. Kitu ninachotaka wakati ujao wa furaha,"alisema.
Alipowasili: Wenger alikuwa hafahamiki wakati anatambulishwa Uwanja wa Highbury (sasa Emirates) Septemba mwaka 1996
Wakati wa furaha: Wenger akiwa ameshika taji la ubingwa wa Ligi Kuu wakati Nahodha, Tony Adams akiwa ameshika Kombe la FA baada ya Arsenal kushinda mataji mawili msimu wa 1997-1998
0 comments:
Post a Comment