// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AISHI MANULA KIBOKO YA YANGA ASEMA; “MECHI YA JANA SITASAHAU” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AISHI MANULA KIBOKO YA YANGA ASEMA; “MECHI YA JANA SITASAHAU” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    AISHI MANULA KIBOKO YA YANGA ASEMA; “MECHI YA JANA SITASAHAU”

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KIPA Aishi Salum Manula wa Azam FC amesema kwamba mechi ya jana dhidi ya Yanga SC itabaki katika kumbukumbu zake, kwani aliokoa michomo mingi na hata bao alilofungwa alipigana kuokoa, ingawa wapinzani walifanikiwa kufunga.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1, Aishi alisema kwamba ulikuwa mchezo mgumu ambao alilazimika kuokoa hatari muda wote wa mchezo.
    Kazi ngumu; Aishi akigaagaa huku akiugulia maumivu baada ya kuumia katika moja ya heka heka za mechi ya jana

    “Lile bao nililofungwa niliucheza ule mpira mara mbili sijui, unarudi watu wetu wanachelewa kuosha, Yanga wanajaribu tena hadi wakafunga, nitalala hoi leo, ila nashukuru hatukufungwa,”alisema.
    Pamoja na kufungwa bao gumu dakika ya 14 na Didier Kavumbangu, lakini pia Aishi alipangua mkwaju wa penalti wa Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 69 kufuatia beki Said Mourad ‘Mweda’ kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. 
    Azam ilisawazisha bao dakika ya 83 kupitia kwa Kevin Friday aliyeipokea vyema pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kumchambua kipa mkongwe Juma Kaseja.
    Azam FC sasa inajiongezea pointi moja na kufikisha pointi 44 baada ya mechi 20, wakati Yanga SC inatimiza pointi 40 baada ya mechi 19.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AISHI MANULA KIBOKO YA YANGA ASEMA; “MECHI YA JANA SITASAHAU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top