Na Prince Akbar, Windhoek, Namibia
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kurejea nchini kesho jioni huku Nahodha wake Aggrey Morris akieleza kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wote.
Nahodha huyo aliyasema hayo Jijini Windhoek na kusema kuwa matokeo ya sare ya 1-1 yalikuwa mazuri ukizingatia kuwa walikuwa ugenini na pia walikosa wachezaji wengi waliozoeleka.
“Licha ya kukosa baadhi ya wachezaji kila mtu kwenye kikosi alijituma na ndio maana tukaweza kupata matokeo kama haya….kwa kweli mimi kama nahodha nimeridhika na najua tutaendelea kufanya vizuri zaidi,”alisema.
Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Ijumaa saa moja kasorobo jioni kwa Shirika la Ngege la Afrika Kusini (SAA).
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kilikwenda sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa Namibia,katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado hazijafungana,na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni,Ramadhani Singano na juma Luizio,na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Atanas Mdam na Hamis Mcha.
Stars ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 kwa mkwaju wa kona uliopigwa na Hamisi Mcha aliyetokea benchi na mpira kuingia moja kwa moja bila kuguswa.
Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya 95 lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni,baada ya kupigwa mpira wa adhabu.
Refa wa mechi hiyo aliingia lawamani kwa kuzidisha muda kupita kiasi kwani mwamuzi wa mezani alionesha dakika tano za nyongeza lakini muamuzi alichezesha dakika tano nyingine hivi kuwawezesha Namibia kupata bao.
Naye Mwalimu Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana.
Kocha wa Namibia Ricardo Manenti aliimwagia sifa Taifa Stars kwa kiwango kilichooneshwa na kusema yeye binafsi ana heshima kubwa kwa timu ya Tanzania.
Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.

Stars ya sasa safi; Nahodha wa timu ya taifa, Aggrey Morris amesema timu ilicheza vizuri jana Namibia |

0 comments:
Post a Comment