Na Prince Akbar, Dar es Salaam
UNAKUMBUKA baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Novemba 7, mwaka jana, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi alisema kikosi chake kisingelisajili wala kuuza mchezaji yeyote? Kwa nini ameamua kusaliti alichokinena na kuamua kusajili mchezaji mmoja?
Siku chache kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo msimu huu Jumapili Desemba 15, mwaka jana, uongozi wa timu ya Rhino Rangers ya Tabora uliamua kutema baadhi ya nyota wake kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni 'kukiuka maadili ya timu hiyo inayoendeshwa kwa misingi na taratibu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kibaya zaidi, rungu hilo likamwangukia mshambuliaji aliyefanya kazi kubwa msimu uliopita kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu, Saad Kipanga aliyefunga mabao 12 katika mechi 14 za Ligi Daraja la Kwanza na kuirejesha kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Vodacom katika Mkoa wa Tabora tangu mwaka 1999 Milambo FC iliposhuka daraja.
"Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom nilitamka wazi kwamba Mbeya City haitauza wala kusajili mchezaji mpya, lakini nilibadili mawazo siku chache baada ya kuona mchezaji muhimu kwa kikosi changu," anasema Mwambusi.
"Kipanga ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, ndiyo maana nikafuta kauli yangu na kumsajili mara moja baada ya kupata nafasi hiyo. Tulikuwa naye kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kisiwani Pemba na alicheza vizuri.
"Sasa nina kikosi kizuri ambacho timu yoyote tunayocheza nayo lazima ijipange hasa sehemu ya ulinzi maana Kipanga ameongeza nguvu katika safu yetu ya ushambuliaji," anasema zaidi Mwambusi.
Kipanga (23), mwenye rekodi ya kuifunga Simba mabao matatu katika mechi tatu mfululizo mwaka jana, huku akiibuka mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita akifunga mabao 12 katika mechi 14, anasema anaamini atafanya vizuri zaidi akiwa na kikosi cha Mwambusi kilichoonyesha ushindani mkali mzunguko wa kwanza na kumaliza nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi.
Uwezo wake wa kukimbia kwa kasi, kukaba na mashuti yake makali ni moja ya sifa zilizomfanya awe lulu katika kikosi hicho cha Rhino Rangers kilichokuwa chini ya kocha aliyetimuliwa, Sebastian Nkoma.
Ni mshambuliaji hatari, ambaye mabeki wa Yanga kwa sasa: Kelvin Yondani, Nadir Haroub Cannavaro', Oscar Joshua na Mbuyu Twite hawana budi kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanamchunga asipate hata nafasi moja ya kupiga shuti kwani kosa moja kwa mkali huyo litawagharimu.
Tangu atue Mbeya City, Mwambusi amwekuwa akimpa nafasi kipindi cha pili akiwa ameshasoma upungufu wa wapinzani. Katika mechi yao ya kwanza mzunguko wa pili waliyoshinda 1-0 dhidi ya 'Wakatamiwa wa Kagera' Kagera Sugar Januari 25 mwaka huu, Kipanga aliingia kipindi cha pili na kupika bao hilo lililopachikwa na Swita Julius.
Pengine, jina la Kipanga si zuri kusikika kwenye masikio ya mashabiki wa Simba hasa mkoani Tabora kutokana na historia ya kuwafunga katika kila mechi ambayo Simba imecheza dhidi ya maafande hao JWTZ mwaka jana.
Kipanga aliifunga Simba katika mechi tatu mfululizo ambazo Rhino na Simba zilikutana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mwaka jana. Katika mechi ya kwanza ambayo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kwenye uwanja huo uliojengwa 1987, Kipanga ndiye aliifungia bao Rhino katika dakika ya 43 akisawazisha bao la penalti lililofungwa na Ramadhani Singano 'Messi' dakika ya 35.
Julai 9 mshambuliaji huyo wa zamani wa Klabu ya Royal FC de Muramvya inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi, pia alifunga bao pekee la Rhino katika mechi yao ya pili ya kujiandaa kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara waliyolala 3-1 dhidi ya 'Wanamsimbazi' kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuketisha watazamaji 30,000.
Mzaliwa huyo wa Nzega, Tabora ndiye aliyefuta ndoto za Simba kuuanza msimu huu kwa ushindi baada ya kuifungia timu yake bao la pili na la kusawazisha kwenye mechi yao ya ufunguzi iliyomalizika kwa sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora Agosti 24, mwaka jana.
CHIMBUKO LAKE KISOKA
Kipanga aliyezaliwa Julai 5, 1990 Nzega, Tabora, anasema alianza kusakata soka akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nyasa One (1) iliyopo Nzega (2000- 2006) na kwamba kipaji chake kilionekana zaidi 2007 alipojiunga na shule ya sekondari Tarime ya mkoani Mara.
"Nikiwa kidato cha pili 2008 nilishiriki michuano ya Copa Coca-Cola nikiwa na timu ya Mkoa wa Tabora. Baada ya mashindano hayo kumalizika, nilichaguliwa kujiunga na kikosi cha kocha Sylivester Marsh cha timu ya taifa ya vijana chini umri wa miaka 17 (U17)," anasema Kipanga.
"Nakumbukua tulikwenda Sudan kushiriki mashindano ya U17 ya Cecafa (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) na tuliporejea nilijiunga na kikosi cha U-20 cha African Lyon wakiniahidi kunipeleka kwenye shule ya vipaji ya michezo ya Makongo, lakini ilishindikana na ikabidi nirudi Tarime," anaongeza.
Mtoto huyo pekee kwenye familia ya Halfan Kipanga, anasema baada ya kupata alama zisizoridhisha kwenye mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2010, ilibidi ategemee soka kuendesha maisha yake.
Anasema 2011 alishiriki mashindano ya Taifa Cup akiwa na timu ya Mkoa wa Tabora na kwamba baada ya mashindano hayo alianza kukipiga katika Ligi Kuu ya Burundi akiwa na Klabu ya Royal FC de Muramvya.
"Nawajua vizuri Amisi Tambwe (Simba) na Didier Kavumbagu (Yanga) kwa sababu nimecheza nao Burundi ingawa nilicheza kwa nusu msimu (miezi sita) nikaamua kurejea nyumbani baada ya kukubaliana 'vitu' vizuri na uongozi wa Rhino," anasema.
Kipanga, ambaye pia hupenda kucheza mpira wa kikapu, ameifungia Rhino mabao matano katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo na hakuwika sana kutokana na majeraha yaliyomkumba katikati mwa mzunguko huo.
ANA NGEKEWA NA SIMBA
"Nahisi nina ngekewa na Simba ndiyo maana nimewafunga katika mechi zote tatu tulizokutana nao, hawakuwa na safu nzuri ya ulinzi mzunguko wa kwanza. Lengo langu ni kufunga mabao mengi zaidi ili niitwe katika timu ya taifa. Hivyo sitaishia kuifunga Simba pekee, timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu zijiandae," anasema Kipanga.
"Niko tayari kusajiliwa na timu kubwa nchini lakini malengo yangu ni kucheza soka la kulipwa Ulaya maana soka letu ni fitina tu. Kwa sasa inabidi kupambana kuhakikisha Mbeya City inanyakua ubingwa," anasema zaidi nyota huyo.
MAISHA BINAFSI
Kipanga, ambaye 2012 alijiunga na Kikosi cha 821 KJ mkoani Kigoma kwa ajili ya mafunzo ya miezi mitatu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), anasema anachukia ulevi na ugomvi.
Ana mke (Therezia Mashaka) na mtoto (Zuena). Anasema anapenda kukaa na familia yake wakati wa mapumziko wakila ugali na maharage huku wakishushia na juisi.

Saad Kipanga katikati akiwatoka viungo wa Simba SC, Amri Kiemba kulia na Saiod Ndemla kushoto, hapa ni wakati akiichezea Rhino Rangers ya Tabora |

0 comments:
Post a Comment