Na Mwandishi Wetu, Moroni
MSAFARA wa timu ya Yanga SC ya Dar es Salaam leo mchana umepata fursa ya kumtembelea Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Chabaka Kilumnaga kufuatia mwaliko wa timu pamoja na viongozi katika hafla ya chakula cha mchana nyumbani kwake eneo la Itsandra Moroni.
Katika hafla hiyo Balozi Chabaka alishukuru timu ya Yanga kwa kufika nyumbani kwake na kujumuika katika chakula cha mchana pamoja na maofisa wa ubalozi waliopo nchini Comoro na Watanzania wengine wanaoishi kwenye kisiwa hicho cha Ngazija.
Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Dk Ahmed El Balidou na Waziri wa Elimu nchini Comoro nao pia walikuwepo ambao kwa pamoja waliukaribisha msafara wa Yanga na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
“Nawakaribisha sana hapa Comoro mjisikie kama mpo nyumbani Tanzania, pili nilifurahishwa na ushindi katika mchezo wa jana ambao niliuhudhuria na mkaweza kuibuka na ushindi, hiyo ilikuwa inaendeleza sifa nzuri ya Yanga pamoja na nchi ya Tanzania kwa ujumla,”alisema Chabaka.
Aidha, Balozi Chabaka alisema anaitakia kila la kheri Yanga katika mchezo wake unaofuata dhidi ya Al Ahly na kusema timu hiyo ina nafasi nzuri ya kufanya vizuri na kusonga mbele kwa kuwang'oa vigogo hao wa soka barani Afrika.
Mkuu wa msafara wa Yanga SC, Ramadhani Nassib ambaye ni Mjumbe Mteule wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliushukuru ubalozi wa kuikaribisha Yanga nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana na kuwatakia maisha mema na yenye mafanikio nchini Comoro ambapo ndio kwanza Ubalozi umeanza miezi mitatu iliyopita.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’ alimshukuru Balozi Chabaka kwa jana kuja uwanjani kuipa sapoti timu na leo kwa kuialika kwa ajili ya chakula cha mchana.
Yanga itandoka kesho kurejea nchini Tanzania majira ya Saa 6:30 mchana kwa ndege na itafika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Saa 8:00 mchana.
Yanga jana ilihitimisha vyema Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuichapa Komorozine mabao 5-2, hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 12-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 7-0 Dar es Salaam na sasa itakutana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly mwezi ujao.

0 comments:
Post a Comment