// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Tuesday, February 18, 2014

        WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA

        Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
        WACHEZAJI watatu wanaocheza soka nchini Tanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
        Mchezaji Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
        Wanaongezeka; Thomas Ulimwengu kushoto anacheza TP Mazembe ya DRC, idadi ya Watanzania wanaocheza nje sasa itaongezeka

        Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
        TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania itatoa ITC hizo.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry