// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YA MALINZI ISIGEUZWE KUWA PAGALA LA MANAZI WA SIMBA NA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YA MALINZI ISIGEUZWE KUWA PAGALA LA MANAZI WA SIMBA NA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 02, 2014

    TFF YA MALINZI ISIGEUZWE KUWA PAGALA LA MANAZI WA SIMBA NA YANGA

    RAIS wa zamani wa Yanga SC, Tarimba Abbas ni miongoni mwa wateule wapya wa Kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo zilizoundwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kutangazwa jana.
    Tarimba, ambaye kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu kama Mwenyekiti, akiwa na Wajumbe Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.

    Kamati ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
    Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
    Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
    Kabla ya hapo, TFF chini ya rais wake, Jamal Malinzi iliwateua Richard Sinamtwa, Ramadhan Nassib, Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama kuingia kwenye Kamati ya Utendaji kama Wajumbe wa kuteuliwa.
    Aidha, TFF iliunda Kamati mbalimbali, zikiwemo Fedha na Mipango inayoongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
    Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
    Kamati ya Soka ya Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
    Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
    Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
    Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
    Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
    Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.
    Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.
    Wajumbe wengi walioteuliwa katika Kamati hizi ni watu ambao ama walikuwa viongozi wa klabu za Simba na Yanga SC au bado viongozi wa klabu hizo hadi sasa. Na zaidi, wengine hata ambao hawapo tena kwenye timu hizo, wameendelea kujihusisha na shughuli za klabu hiyo kutokana na mapenzi yao.
    Naamini, wengi wetu tunafahamu Simba na Yanga ni muhimu katika soka yetu, lakini ushabiki wake unapoingizwa katika sekta muhimu kama TFF ni hatari kwa mchezo huo hapa nchini.
    Usimba na Uyanga unapoingia TFF unaleta mgawanyiko na hatari yake kubwa ni kuleta vurugu katika soka yetu. Tumekwishaona sana athari za kuwa na viongozi mashabiki ndani ya TFF, hawa mara nyingi wanakwenda kuwa vibaraka wa klabu zao, badala ya kwenda kufanya kazi kwa maslahi ya mchezo huo nchini.
    Desemba 21, mwaka jana baada ya Simba SC kuifunga Yanga mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, tulimuona Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, namna alivyojitoa kusherehekea ushindi wa Wekundu wa Msimbazi.
    Kaburu alivalia jezi ya Simba SC yenye kuwakejeli Yanga na kipigo cha 5-0 na kumdhihaki Emmanuel Okwi aliyehamia Yanga na akashiriki kikamilifu sherehe za ubingwa wa Simba, ikiwemo kuvalishwa Medali na Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambazo walivalishwa Simba SC.
    Wakati Malinzi anamvalisha Medali hiyo Kaburu aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, nilijiuliza na siku ya Yanga wakishinda itakuwaje kwa Rais huyo wa TFF, maana naye amewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo ya Jangwani.
    Na nikajiuliza zaidi, kama hiyo ndiyo picha ya viongozi wetu wapya, pale TFF patakuwaje? Na ile dhamira ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya soka yetu itawezekana kweli?
    Wakati bado natafakari haya, jana inaundwa Kamati kuna watu wengine waliowahi kuongoza Simba na Yanga, tena wakiwemo ambao wamekwishaonyesha misimamo ya kinazi haswa kiasi cha kufikia kukiuka hata taratibu za mchezo na kusababisha uvunjifu wa amani viwanjani.
    Machi 31, mwaka 2002 Simba iliifunga Yanga 4-1 katika Fainali ya Kombe la Tusker Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini almanusra mchezo huo uliohudhuriwa na rais mstaafu, Ally Hassan Mwinyi uvunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka Selemani kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
    Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. 
    Baada ya hapo, Tarimba alifungiwa na TFF wakati huo Chama cha Soka Tanzania, FAT), kabla ya baadaye kuamua kuachana kabisa na mambo ya soka na kuingia kwenye siasa, huku akiendelea shughuli zake nyingine.
    Kama kweli tunataka kuleta mabadiliko na maendeleo katika soka yetu, lazima tuepuke kuwa na watu ambao wataendekeza unazi wa Simba na Yanga badala ya kufanya kazi za soka.
    Lakini Malinzi amejiingiza kwenye mtego mbaya kwa kulundika watu wengi wa Simba na Yanga pale TFF, ambao mwisho wa siku watataka kutumia chombo kile kwa maslahi ya klabu zao. Hii ni hatari na lazima sana Malinzi azungumze na watu aliowateua kuwakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na haki, bila kuingiza utashi na mapenzi ya klabu zao, vinginevyo itakuwa vurugu tupu. Jumapili njema. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YA MALINZI ISIGEUZWE KUWA PAGALA LA MANAZI WA SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top