// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAMBWE: ILE HAT TRICK ILIKUJA YENYEWEEEE, SASA WATANITAMBUA VIZURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAMBWE: ILE HAT TRICK ILIKUJA YENYEWEEEE, SASA WATANITAMBUA VIZURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 02, 2014

    TAMBWE: ILE HAT TRICK ILIKUJA YENYEWEEEE, SASA WATANITAMBUA VIZURI

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MSHAMBULIAJI Mrundi Amisi Tambwe wa Simba amesema hakutegemea kufunga mabao matatu peke yake 'hat-trick' katika mchezo wao wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara waliopata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya 'maafande'a Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Simba imefufua ndoto zake za kufanya vizuri msimu huu baada ya kuwashindilia mabao hayo maafande hao wanaonolewa na kocha mpya, Hemed Morocco, ambaye mzunguko wa kwanza alikuwa akikifua kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union. Shukrani kwa mabao ya kiungo Jonas Mkude dakika ya 10 na Tambwe dakika za 22, 28 na 50.
    Huu hapa; Amisi Tambwe akiwaonyesha mashabiki mpira baada ya kukabidhiwa (pichani chini anakabidhiwa na refa) kwa kufunga mabao matatu peke yake jana Simba SC ikishinda 4-0


    Akizungumza na BIN ZUBEIRY mara tu baada ya kukabidhiwa mpira wake kwa kukipa hat-trick na refa Nathan Lazaro kutoka Kilimanjaro, Tambwe aliyeonekana mwenye furaha tele, alisema hakutarajia kuona timu yake ikiibuka na ushindi huo mnono kwa vile maafande hao wana timu ngumu kuruhusu nyavu zake kuitikishwa.
    "Kwa kweli sikutegemea kufunga hat-trick katika mechi ya leo, unajua hawa jamaa (Oljoro JKT) wana timu nzuri ambayo si rahisi kufungika. Tulicheza nao Arusha tyukawafunga goli moja tu nami sikufunga, nakumbuka walipata penalti siku hiyo (Agosti 28 mwaka jana) lakini bahati mbaya wakakosa," amesema Tambwe.
    "Sijui wamejisahau vipi leo ... sikutarajia kufunga hat-trick kabisa ndiyo maana nimeshangilia sana baada ya kufunga bao la nne kwa timu yangu. Nafikiri kujituma kwanga na timu kwa ujumla mazoezini ndiko kumetufikisha hapa.
    "Unajua nafanya mazoezi kwa nguvu na nafunga sana mazoezini, natumaini nitafanya vizuri zaidi katika michezo inayofuata ili kuisaidia timu kupata mafanikio," amefafanua zaidi Tambwe, ambaye baada ya kukamilisha hat-trick yake amenaswa na kamera za BIN ZUBEIRY akirukaruka kushangilia.
    Hat-trick hiyo pengine imemwondolea ngundu nyota huyo ambaye alikuwa hajafunga goli hata moja katika michezo nane aliyokichezea kikosi cha Kocha Mcoaratia Zdravko Logarusic tangu afunge mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga katika mchezo wa 'Nani Mtani Jembe' uliopigwa Uwanja wa Taifa Desemba 21 mwaka jana.
    Baada ya mchezo huo uliofukuizisha benchi zima la ufundi la Yanga lililokuwa linaongozwa na Mholanzi Ernie Brandts, Simba ilicheza mechi nane: sita za mashindano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzabar, moja ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar waliyofungwa 1-0 na moja ya ligi dhidi ya Rhino Rangers wakishinda 1-0 lakini mkali huyo wa kufumania nyavu -- Tambwe alikuwa hajapachika hata bao moja.
    Mabao matatu ya jana, yamemfanya Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana, kufikisha idadi ya mabao 13 katika ligi hiyo msimu huu, matatu mbele ya mfungaji bora wa msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast. 
    Kabla ya mechi ya jana, Tchetche aliyefunga mabao yote mawili katika ushindi mwembamba wa 1-0 ambao Azam FC imeupata katika mechi mbili mfululizo za mzunguko wa pili dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar Januari 25 na Rhino Rangers Jumatano, alikuwa na mabao 10 sawa na Tambwe.  
    Ushindi huo unaifanya Simba iliyopata ushindi katika mechi mbili mfululizo za mzunguko wa pili ifikikshe pointi 30 baada ya kucheza mechi 15 katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi, pointi moja nyuma ya wababe Mbeya City, mbili nyuma ya Yanga na tatu Azam FC walioko kileleni. 
    Kabla ya kujiunga na Simba msimu huu akitokea Klabu ya Vital'O ya Burundi aliyoipa ubingwa wa Kombe la Kagame mwaka jana nchini Sudan, Tambwe alikuwa ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Burundi.
    Mabao ya Tambwe na Mkude ya leo yanafanya idadi ya mabao kufikia 230 kwani kabla ya mechi mbili za leo, idadi ya mabao ilikuwa 224. Wachezaji wawili wa Mgambo Shooting, Peter Mwalianzi na Bolly Shaibu pia wamefunga bap moja kila mmoja katika ushindi wa 2-0 ambao timu yao imeupata dhidi ya 'Wauza Mitumba wa Ilala' Ashanti United kwenye Uwanja wa Azam (Azam Complex) jijini leo jioni.
    Mzunguko wa kwanza yalifungwa mabao 208 huku mshambuliaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana, huku Tambwe akifunga mabao 10 na kuongoza safu ya wafumania nyavu mzunguko wa kwanza. 
    Mshambuliaji wa Coastal ambaye hakufunga hata bao moja mzunguko wa kwanza, Mganda Lutimba Yayo ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo akiifungia timu yake bao la dakika ya nne tu ya mchezo wao wa kwanza waliolazimishwa sare ya bao moja na maafande wa OPljoro JKT nyumbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Januari 25.
    Aidha, hakuna mchezaji aliyefunga bao kwa njia ya penalti mzunguko wa pili ambao mpaka sasa penalti moja tu imeshatolewa kwa Simba katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rhino walioshinda 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili. Kiungo aliye katika kiwango cha juu cha soka, Ramadhani Singano 'Messi' licha ya kuuifungia Simba bao hilo la ushindi alikosa penalti hiyo. Mpigaji wa penalti wa Simba kwa sasa, 
    Tambwe alikuwa ametolewa na kocha Logarusic wakati tuta hilo likitolewa. Katika mabao yake 10, Tambwe amefunga mabao matatu kwa njia ya penalti. Jerry Santo ndiye anaoongoza kwa kuwa na mabao mengi zaidi ya penalti. Mkenya huyo aliifungia Coastal mabao manne kwa njia hiyo mzunguko wa kwanza.
    Jumla ya penalti 25 zimeshatolewa na marefa wa ligi hiyo msimu huu, 24 zikiwa ni za mzunguko wa kwanza. Penalti zilizofungwa ni 20 huku wachezaji wanne wakiungana na Messi kwa kukosa penalti mzunguko wa kwanza. Wachezaji hao ni Stanley Nkomola (JKT), Babu Ally (Oljoro), Elius Maguri (Ruvu) na Jeremiah Juma (Prisons).
    Winga hatari wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa, ndiye mchezaji anayeonekana kuwa hatari zaidi na pengine ndiye mchezaji bora wa ligi hiyo kwa takwimu zilizopo. Katika michezo saba ya mzunguko wa kwanza ambayo mchezaji huyo wa zamani wa Kahama United, Kagera Sugar, Azam FC na Simba aliichezea Yanga, alifunga mabao sita na kupika mabao mengine sita.  
    Mzaliwa huyo wa Mwanza, hakucheza michezo mitano ya mwanzo kutumikia adhabu ya kukosa mechi sita aliyopewa na Shirikisho la Soka (TFF) baada kubainika kuwa alijisajili katika klabu mbili za Simba na Yanga kuzitumikia msimu huu.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMBWE: ILE HAT TRICK ILIKUJA YENYEWEEEE, SASA WATANITAMBUA VIZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top