GUMZO kubwa katika soka ya Tanzania kwa sasa ni kuhusu mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi ambaye amesajiliwa na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam wakati wa dirisha dogo.
Mapema wiki hii, ziliibuka habari zilizowafurahisha mashabiki wa Yanga SC, kwamba mchezaji huyo ameidhinishwa kuchezea mabingwa hao wa Bara na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katibu wa TFF, Celestine Mwesigwa aliwaambia Waandishi wa Habari kwamba, sakata la Okwi limemalizika na mchezaji huyo sasa yuko huru kucheza.
Ikumbukwe, awali TFF ilituma barua FIFA kuomba ufafanuzi kama inaweza kumuidhinisha mchezaji huyo Yanga SC au la na ingawa majibu ya awali ya Mwesigwa yalikuwa anaweza kuidhinishwa, lakini barua halisi ya bodi hiyo ya soka duniani inatoa majibu tofauti.
Kwa mujibu wa barua hiyo, FIFA haijamruhusu Okwi kuchezea Yanga SC, bali imetoa maelekezo ya TFF kufuata.
BIN ZUBEIRY imefanikiwa kupata nakala ya barua hiyo iliyotumwa nchini Februari 12, mwaka huu kutoka makao makuu ya shirikisho hilo, Zurich kwenda kwa Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa Dar es Salaam na FIFA imesema yenyewe haihusiki na usajili wa mchezaji, bali ni shirikisho la nchi husika.
Barua ya FIFA imeiagiza TFF ifuate kanuni na taratibu za usajili katika suala la mchezaji huyo.
FIFA pia imesema inatambua Okwi alihamishwa kutoka Simba SC Januari 15, mwaka jana kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa Mkataba wa kudumu na baadaye, kufuatia uamuzi wa jaji mmoja baada ya mchezaji huyo kufungua kesi FIFA, aliruhusiwa kuchezea SC Villa ya Uganda kwa muda Oktoba 5, mwaka jana.
FIFA pia imesema inatambua Okwi alihamishwa kutoka SC Villa kujiunga na Yanga SC Desemba 15, mwaka jana, lakini imesistiza TFF ifuate taratibu na kanuni za usajili, tena ikiielekeza vipengele vya kupitia katika kumaliza kesi hiyo.
FIFA pia imesema inatambua Simba SC inadai fedha za kumuuza Okwi Etoile, lakini imesema hiyo ni kesi tofauti na suala la uhalali wa mchezaji huyo Yanga SC.
Ikumbukwe, TFF iliiandikia FIFA kutaka ufafanuzi wa mchezaji huyo kama wanaweza kumhalalisha kuchezea Yanga na baada ya kupokea, majibu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Mwesigwa alizungumza na BIN ZUBEIRY akasema suala hilo limekwisha na mchezaji huyo yuko huru kuchezea Yanga.
Wazi, maelezo ya Mwesigwa yamezingatia maelekezo ya FIFA, wamepitia kanuni na taratibu za usajili ili kuona kama Okwi anaweza kuwa sahihi kuchezea Yanga.
Suala kama la Okwi ufafanuzi wake unapatikana katika kanuni ya tano ya usajili aya ya kwanza hadi ya tatu, ambayo kwa muhtasari inasema mchezaji anaweza kusajili na klabu zisizozidi tatu kwa msimu, lakini ataruhusiwa kuchezea mechi za mashindano katika timu mbili tu.
Okwi alisajiliwa Etoile msimu uliopita na kufika Mei mwaka jana akavurugana na klabu hiyo, akahamia SC Villa mwishoni mwa msimu uliopita.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo ya usajili, Okwi anaweza kuchezea Yanga SC mechi za mashindano msimu huu, kulingana na maelekezo ya FIFA.
Aya ya tatu ya kanuni hiyo inasema; “3. Players may be registered with a maximum of three clubs during one season. During this period, the player is only eligible to play official matches for two clubs,”.
Tafsiri yake; “Mchezaji anaweza kusajiliwa na klabu zisizozidi tatu kwa msimu, lakini katika msimu husika hawezi kuchezea mechi rasmi katika klabu zaidi ya mbili,”.
Sasa mustakabali wa Okwi Yanga utategemea na kesi yake dhidi ya klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, kama atashinda. Iwapo atashindwa na FIFA ikasema huyo ni mchezaji halali wa klabu ya Tunisia, ina maana Yanga itakuwa imeingia hasara kumsajili, lakini kwa sasa Okwi anaweza kucheza Yanga SC.
Sakata la mchezaji huyo linaanzia Desemba mwaka juzi aliposaini Mkataba mpya na Simba SC wa miaka miwili mjini Kampala, Uganda mbele ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage katika hoteli ya Sheraton.
Baada ya hapo, hakuja Dar es Salaam kuendelea na kazi Simba SC, zikaibuka habari za kuuzwa kwake Tunisia kwa dau la dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh. Milioni 480,000 za Tanzania.
Hata hivyo, Okwi akaingia katika mgogoro na Etoile miezi michache tu baada ya kujiunga nayo, klabu hiyo ikidai mchezaji huyo ni mtoro baada ya kushindwa kurejea kazini, kufuatia kupewa ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa na mshambuliaji huyo akidai klabu hiyo imeshindwa kumlipa mishahara.
Okwi akafungua kesi FIFA ambayo alishinda na kupewa ruhusa ya kuchezea SC Villa kwa muda wakati kesi yake ikiendelea. Wakati huo huo, Etoile ilikuwa haijalipa Simba SC dola 300,000 za kumnunua mchezaji huyo.
Inafahamika, Etoile inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kwa sasa na inawezekana ni kwa kutambua hilo, FIFA ikamruhusu Okwi kuchezea SC Villa.
Na inawezekana mwisho wa siku, Okwi akashinda kesi ya msingi dhidi ya Etoile.
Kwa kutazama kanuni hii na historia ya Okwi ndani ya misimu hii miwili, mchezaji huyo anaweza kucheza Yanga SC.
KUNRADHI: Mapema asubuhi ya leo, niliweka makala hii, ikisema Okwi hawezi kucheza Yanga kwa sababu amekwishacheza Etoile na SC Villa ndani ya msimu mmoja. Lakini Kalenda ya ligi ya Tunisia iko sawa na kalenda ya ligi ya Tanzania Bara, inaanza kati ya Agosti na Septemba na kumalizika Mei. Kwa kuwa Okwi hajacheza Tunisia tangu Mei mwaka jana, hivyo kwa mujibu wa sakata lake na kanuni ya FIFA, yuko huru kucheza Yanga. Ninaomba radhi kwa usumbufu wowote niliosababisha. Yalikuwa ni makosa ya kibinadamu na hayakuwa na lengo lingine lolote, zaidi kutaka kuisaidia Yanga yenyewe isijiingize matatani. Asanteni.

0 comments:
Post a Comment