• HABARI MPYA

    Tuesday, February 04, 2014

    MANJI AMWAGA MAMILIONI TFF KUSAIDIA MENDELEO YA SOKA, 40 WATEULIWA KUNG’AMUA VIPAJI UBORESHAJI TAIFA STARS

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    KAMPUNI ya Quality Group Limited, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC, Yussuf Manji imetoa Sh. Milioni 10 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuunga mkono mikakati ya shirikisho la katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
    Mchango huo wa Quality Group utatumika katika programu mbalimbali za kuendeleza mpira wa miguu nchini ambapo tunaishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono mikakati yetu.
    Asante bosi; Kampuni ya Quality Group ya Yussuf Manji imetoa msaada wa Sh. Milioni 10 TFF kusaidia michakato ya maendeleo ya soka

    Katika hatua nyingine, TFF imeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
    Makocha hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
    Walioteuliwa ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri (Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani (Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
    Elly Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es Salaam).
    Kenny Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera (Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).
    Peter Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Sebastian Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan (Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es Salaam),
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI AMWAGA MAMILIONI TFF KUSAIDIA MENDELEO YA SOKA, 40 WATEULIWA KUNG’AMUA VIPAJI UBORESHAJI TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top