BAADA ya kuadhiriwa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester City imerejea kwenye wimbi la ushindi baada ya kuilaza 1-0 Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad usiku huu.
City ilishindwa kufunga bao hata moja katika mechi zao tatu zilizopita kati ya nne na hadi mapumziko leo ilikuwa haijapata bao.
Manuel Pellegrini akawaingiza Jeses Navas na Stevan Jovetic kipindi cha pili na hapo ndipo ilipopata ushindi, kufuatia bao la Yaya Toure dakika ya 70, ambalo linakuwa bao lake la 16 msimu huu.
Matokeo hayo yanafanya City ibaki inazidiwa pointi tatu tu vinara wa Ligi Kuu Chelsea, ingawa kikosi cha Manuel Pellegrini kina mchezo mmoja mkononi.
Toure (kulia) akiwatoka mabeki wa Stoke kabla ya kufunga
0 comments:
Post a Comment