Na Dina Ismail, Dar es Salaam
WAKATI Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiendelea leo jioni kwa mechi mbili Simba inawakaribisha 'maafande' wa Oljoro JKT Uwanja wa Taifa huku 'Wauza Mitumba wa Ilala', Ashanti United wakiwavaa maafande wengine wa Mgambo Shooting kutoka Tanga kwenye Uwanja wa Azam (Azam Complex jijini Dar es Salaam, jumla ya mabao 16 yamefungwa katika mechi 10 za mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Idadi hiyo inafanya magoli yalifungwa katika ligi hiyo msimu huu kufikia 224 kwani mzunguko wa kwanza yalifungwa mabao 208 huku mshambuliaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana, Mrundi Amisi Tambwe akifunga mabao 10 na kuongoza safu ya wafumania nyavu mzunguko wa kwanza.
Tayari mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita Kipre Herman Tchetche wa Azam FC ameshapachika mabao mawili katika mechi mbili za mzunfguko wa pili walizoshinda 1-0 dhidi ya mabiongwa wa 199 na 2000, Mtibwa Sugar Januari 25 na 1-0 dhidi ya Rhino Rangers Jumatano akifikisha idadi ya mabao 10 na kumkamata Tambwe kileleni.
Mshambuliaji wa Coastal ambaye hakufunga hata bao moja mzunguko wa kwanza, Mganda Lutimba Yayo ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo akiwafungia mabingwa hao wa Tanzania Bara 1988 bao la dakika ya nne tu ya mchezo wao wa kwanza waliolazimishwa sare ya bao moja na maafande wa OPljoro JKT nyumbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Januari 25.
Aidha, hakuna mchezaji aliyefunga bao kwa njia ya penalti mzunguko wa pili ambao mpaka sasa penalti moja tu imeshatolewa kwa Simba katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rhino walioshinda 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili. Kiungo aliye katika kiwango cha juu cha soka, Ramadhani Singano 'Messi' licha ya kuuifungia Simba bao hilo la ushindi alikosa penalti hiyo. Mpigaji wa penalti wa Simba kwa sasa,
Tambwe alikuwa ametolewa na kocha Mcroatia Zdravko Logarusic wakati tuta hilo likitolewa. Katika mabao yake 10, Tambwe amefunga mabao matatu kwa njia ya penalti. Jerry Santo ndiye anaoongoza kwa kuwa na mabao mengi zaidi ya penalti. Mkenya huyo aliifungia Coastal mabao manne kwa njia hiyo mzunguko wa kwanza.
Jumla ya penalti 25 zimeshatolewa na marefa wa ligi hiyo msimu huu, 24 zikiwa ni za mzunguko wa kwanza. Penalti zilizofungwa ni 20 huku wachezaji wanne wakiungana na Messi kwa kukosa penalti mzunguko wa kwanza. Wachezaji hao ni Stanley Nkomola (JKT), Babu Ally (Oljoro), Elius Maguri (Ruvu) na Jeremiah Juma (Prisons).
Winga hatari wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngasa, ndiye mchezaji anayeonekana kuwa hatari zaidi na pengine ndiye mchezaji bora wa ligi hiyo kwa takwimu zilizopo. Katika michezo saba ya mzunguko wa kwanza ambayo mchezaji huyo wa zamani wa Kahama United, Kagera Sugar, Azam FC na Simba aliichezea Yanga, alifunga mabao sita na kupika mabao mengine sita.
Mzaliwa huyo wa Mwanza, hakucheza michezo mitano ya mwanzo kutumikia adahbu ya kukosa mechi sita aliyopewa na Shirikisho la Soka (TFF) baada kubainika kuwa alijisajili katika klabu mbili za Simba na Yanga kuzitumikia msimu huu.

0 comments:
Post a Comment