Na Salum Vuai, ZANZIBAR
NDOTO za Wazanzibari kuziona timu zao zikisonga mbele katika mashindano ya klabu barani Afrika, zimefutika kabisa baada ya jioni ya leo KMKM kutolewa katika kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa.
Licha ya wanamaji hao kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dedebit FC ya Ethiopia katika pambano la marudiano lililochezwa uwanja wa Amaan, haikusaidia kuivusha timu hiyo zaidi ya kulinda heshima kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani.
KMKM inayonolewa na kocha mkuu Ali Bushiri ilihitaji zaidi ya mabao matatu kusonga mbele, au angalau kupata sare na kusubiri hatima kupitia mikwaju ya penelti.
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Zanzibar msimu uliopita, walianza kucheka na nyavu mapema katika dakika ya tatu ya mchezo, kwa bao lililofungwa na Maulid Kapenta baada ya kuwekewa pasi murua na Juma Mbwana.
Bao hilo liliwafanya wachezaji wa timu hiyo waongeze kasi, lakini walishindwa kuzitumia nafasi nyingi za kufunga walizozipata katika kipindi cha kwanza.
Washambuliaji wa timu hiyo akina Mudrik Muhibu, Iddi Kambi, Juma Mbwana na Maulid Kapenta, walishirikiana vyema kufanya mashambulizi lakini wakaishia kupiga mipira butu langoni.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, KMKM ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kasi ya KMKM katika kipindi cha pili ilipungua kidogo, ambapo wachezaji wa Ethiopia walitawala sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikuweza kuzaa mabao.
Katika dakika ya 63, wachezaji Shimeket Gugsa na Dawit Fekadu, walikwenda vyema na mpira, kabla kumpasia Gabriel Ahmed ambaye shuti lake lilidakwa kifundi na mlinda mlango wa KMKM Mudathir Khamis.
KMKM ilizinduka na kuanza kujipanga upya, na katika dakika ya 56, wachezaji wake walifanya shambulizi kubwa na kufanikiwa kuandika bao la pili lililowekwa nyavuni na Mudrik Muhibu.
Hata hivyo, kasi ya mabaharia hao kupata mabao zaidi, iliathiriwa katikati ya kipindi cha pili baada ya mchezaji wake Khamis Ali kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya.
Kwa matokeo hayo, Dedebit inaingia hatua ya pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
Na habari kutoka Beira nchini Msumbiji, zimefahamisha kuwa, wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Azam FC, imefungishwa virago baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Ferroviario Da Beira katika mchezo wa marudiano.
Azam ilishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, na hivyo imetolewa kwa mabao 2-1.

Wachezaji wa KMKM na Dedebit wakionyeshana kazi leo Uwanja wa Amaan |
KMKM inayonolewa na kocha mkuu Ali Bushiri ilihitaji zaidi ya mabao matatu kusonga mbele, au angalau kupata sare na kusubiri hatima kupitia mikwaju ya penelti.
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Zanzibar msimu uliopita, walianza kucheka na nyavu mapema katika dakika ya tatu ya mchezo, kwa bao lililofungwa na Maulid Kapenta baada ya kuwekewa pasi murua na Juma Mbwana.
Bao hilo liliwafanya wachezaji wa timu hiyo waongeze kasi, lakini walishindwa kuzitumia nafasi nyingi za kufunga walizozipata katika kipindi cha kwanza.
Kocha wa KMKM, Ali Bushiri kushoto akisema na wachezaji wake wakati wa mechi leo Uwanja wa Amaan |
Washambuliaji wa timu hiyo akina Mudrik Muhibu, Iddi Kambi, Juma Mbwana na Maulid Kapenta, walishirikiana vyema kufanya mashambulizi lakini wakaishia kupiga mipira butu langoni.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, KMKM ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kasi ya KMKM katika kipindi cha pili ilipungua kidogo, ambapo wachezaji wa Ethiopia walitawala sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikuweza kuzaa mabao.
Katika dakika ya 63, wachezaji Shimeket Gugsa na Dawit Fekadu, walikwenda vyema na mpira, kabla kumpasia Gabriel Ahmed ambaye shuti lake lilidakwa kifundi na mlinda mlango wa KMKM Mudathir Khamis.
KMKM ilizinduka na kuanza kujipanga upya, na katika dakika ya 56, wachezaji wake walifanya shambulizi kubwa na kufanikiwa kuandika bao la pili lililowekwa nyavuni na Mudrik Muhibu.
Hata hivyo, kasi ya mabaharia hao kupata mabao zaidi, iliathiriwa katikati ya kipindi cha pili baada ya mchezaji wake Khamis Ali kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya.
Kwa matokeo hayo, Dedebit inaingia hatua ya pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
Na habari kutoka Beira nchini Msumbiji, zimefahamisha kuwa, wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Azam FC, imefungishwa virago baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Ferroviario Da Beira katika mchezo wa marudiano.
Azam ilishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, na hivyo imetolewa kwa mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment