Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya
ALIPOFIKA Simba SC alichagua jezi namba 17 na jana amefunga bao la 17 tangu ameanza kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam Septemba mwaka jana, akitokea Vital’O ya Burundi.
“Nimefurahi sana, umejuaje? Kweli, hili ni bao la 17 tangu nianze kucheza Simba na ninavaa jezi namba 17,”alisema Tambwe jana Uwanja wa Sokoine baada ya mechi dhidi ya Mbeya City, timu hizo zikitoka sare ya 1-1, yeye akiwasawazishia Wekundu wa Msimbazi dakika ya 50, kufuatia wenyeji kupata la kuongoza mapema kipindi cha kwanza.
Amisi Tambwe, raia wa Burundi amedhihirisha yeye ni mkali kweli wa mabao, kwani katika mechi 23 alizoichezea Simba SC hadi sasa za mashindano yote na za kirafiki, amefunga mabao 17.
Kwa sasa, Tambwe ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao katika Ligi Kuu, akiwa amefunga mabao 15 na anafuatiwa kwa mbali na mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast, mwenye mabao 10.
Tambwe amekuwa kipenzi cha wana Simba SC kutokana na kuweza pia kutikisa nyavu za mahasimu, Yanga SC katika mechi mbili mfululizo baina ya timu hizo.
Tambwe alikuja Simba SC kwa pamoja na Mrundi mwenzake, beki Gilbert Kaze wakitokea wote Vital’O msimu huu, baada ya kung’ara katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame nchini Sudan wakiiwezesha klabu yao kutwaa taji la michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yake.
Hata hivyo, Kaze amepoteza namba katika kikosi cha kwanza tangu ujio wa kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic, ambaye amekuwa akimpanga beki Mkenya, Donald Mosoti aliyetokea naye Gor Mahia ya Kenya. Heshima kwa Tambwe.

Jezi amba 17, mabao 17; Amisi Tambwe jana katika mechi na Mbeya City |

Mkali kweli; Tambwe amecheza mechi 23 tu Simba SC hadi sasa, lakini tayari amefunga mabao 17 |
Hata hivyo, Kaze amepoteza namba katika kikosi cha kwanza tangu ujio wa kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic, ambaye amekuwa akimpanga beki Mkenya, Donald Mosoti aliyetokea naye Gor Mahia ya Kenya. Heshima kwa Tambwe.
0 comments:
Post a Comment