KOCHA Tim Sherwood aliwataka vijana wake wafanye kazi na Emmanuel Adebayor ameiongoza vizuri kazi hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kuifungia Tottenham Hotspur mabao mawili katika ushindi wa 3-1 Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Europa League.
Matokeo hayo yanaifanya Spurs iliyofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza,ipate ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Dnipro na kutinga 16 Bora ya Europa League ambako itakutana na Benfica.
Christian Eriksen alianza kufunga dakika ya 56 kabla ya Mtogo Emmanuel Adebayor kumaliza kazi dakikaza 65 na 69 katika mchezo ambao wageni walimpoteza mchezaji wao, Zozulya aliyetolewa nje kwa nyekundu dakika ya 62, akitoka kuifungia timu hiyo bao dakika ya 48.
Katika mechi nyingine, Valencia imetoka 0 – 0 na Dynamo Kyiv, Trabzonsporimefungwa 2-0 na Juventus, Lyon imeifunga 1 – 0 FC Chornomorets, KRC Genk imefungwa 2-0 na Anzhi Makhachkala, Fiorentina imetoka 1 – 1 na Esbjerg fB, AZ imetoka 1 – 1 na Slovan Liberec na Benfica imeifunga 3 – 0 PAOK Salonika.
Nayo Shakhtar Donetsk imefungwa 2-1 na Viktoria Plzen, Napoli imeifunga 3 – 1 na Swansea City, Ludogorets Razgrad imetoka 3 – 3 na Lazio, Eintracht Frankfurt imetoka 3 – 3 na FC Porto, FC Red Bull Salzburg imeilaza 3 – 1 Ajax, Sevilla imeifunga 2 – 1 NK Maribor, Basel imeichapa 3 - 0 Maccabi Tel Aviv na Rubin Kazan imefungwa 2-0 na Real Betis.
Mkali kweli: Emmanuel Adebayor ameifungia mabao mawili muhimu Spurs na kuivusha Hatua ya 16 Bora ambako itakutana na washindi wa pili wa mwaka jana, Benfica
Kocha Tim Sherwood akipeana saluti na Adebayor baada ya kuifungia Spurs mabao mawili katika ushindi wa 3-1 usiku wa kuamkia leo
0 comments:
Post a Comment