YANGA SC imetoa sare ya bila kufungana na KS Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Albania katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo uliofanyika eneo la Side Manavagat.
Huo ulikuwa mchezo wa tatu kwa Yanga katika ziara yake ya kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Ligi ya Mabingwa, nchini Uturuki na wa pili chini ya kocha mpya, Mholanzi Hans van der Pluijm.
Kikosi cha Yanga leo |
Katika michezo yake miwili ya awali, iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor ikiongozwa na Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa, lakini baada ya kuja Pluijm ikaifunga 2-0 Altay SK na leo 0-0.
Yanga ipo Uturuki tangu Januari 9, mwaka huu na inatarajiwa kurejea nchini Januari 23.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, David Luhende, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa/Said Bahanuzi, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu/Simon Msuva, Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza
0 comments:
Post a Comment