Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni
Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja
‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.
Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka
waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi
ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya
kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa
moja ya tukio hilo la kihistoria.
Mata noma; Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania kushoto akiwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) na washindi wa Awamu ya kwanza ya Airtel Mimi ni Bingwa, kutoka Manchester, England jana. |
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege,
moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson
Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa
ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza
yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni
Bingwa.
“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada
ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza
nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili
kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel
kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza
kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.
Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando
alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka
Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake
waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu
kuiboresha timu.
“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga.
Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili
kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.
Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi
kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni
kama ndoto kwake.
“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson
moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu
kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee
kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya
Airtel,” alisema.
Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu
kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka
Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.
Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya
shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila
mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa
kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu
maswali mengi iwezekanavyo.
Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza
mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam,
Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni
jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo
wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph
Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka
Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison
Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini
Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment