Na Boniface Wambura, Ilala
SHIRIKISHO la Soka Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.
Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.
Kessy na Gumbo wamewahi kuchezea Yanga na wote wanatokea Temeke.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.
Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.
Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.
SHIRIKISHO la Soka Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.
Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.
Salum Kinje sasa anakwenda kucheza Shelisheli |
TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
Rashid Gumbo aliwika Yanga |
Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.
Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.
0 comments:
Post a Comment