Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Stepehn Bengo leo ameiongoza KCC ya Uganda kuwafunga mabao 3-2 wenyeji KMKM katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi 2014, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bengo leo alitamba katika nafasi ya kiungo Uwanja wa Amaan akiiongoza vyema timu yake kupata ushindi huo dhidi ya timu ngumu, KMKM ambao ni mabingwa wa Zanzibar.
Mabao ya KCC yalifungwa na Herman Waswa dakika ya 10, Tony Odur dakika ya 20 na William Waoro dakika a 82, wakati ya KMKM yalifungwa na Hamisi Ali dakika ya saba na Maulid Ibrahim ‘Kapenta’ dakika ya 79.
Kwa ujumla timu zote zilicheza kwa kiwango kisichopishana sana, zaidi KCC walinufaika na udhaifu wa safu ya ulinzi ya KMKM kupata mabao matatu.Kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, Mbeya City imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Clove Stars.
Mbeya City walitangulia kupata bao dakika ya 13, mfungaji Deus Kaseke na Mohamed Juma Mtwanga akawasawazishia Clove dakika ya 24.
Mchezo wa pili wa Kundi B kati ya Simba SC na AFC Leopard ya Kenya utafuatia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Amaan.
Katika mchezo huo mchezaji wa timu ya KMKM Khamis Ali alipewa zawadi ya King’amuzi cha Azam TV na dishi lake kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika nyasi bandia za uwanja wa Amaan.
Wakati huo huo: Msemaji wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi, Farouk Karim amesema kwamba kufuatia kujitoa kwa Yanga SC, timu ya Ashanti United ya Ilala imechukua nafasi hiyo.
Farouk amesema Ashanti itawasili hapa kesho na usiku itamenyana na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, ambao utatanguliwa na mechi kati ya Azam FC na Spice Stars Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mshambuliaji wa KCC, William Waoro akifunga bao la ushindi la timu yake leo Uwanja wa Amaan. |
Mabao ya KCC yalifungwa na Herman Waswa dakika ya 10, Tony Odur dakika ya 20 na William Waoro dakika a 82, wakati ya KMKM yalifungwa na Hamisi Ali dakika ya saba na Maulid Ibrahim ‘Kapenta’ dakika ya 79.
Kwa ujumla timu zote zilicheza kwa kiwango kisichopishana sana, zaidi KCC walinufaika na udhaifu wa safu ya ulinzi ya KMKM kupata mabao matatu.Kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, Mbeya City imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Clove Stars.
Mbeya City walitangulia kupata bao dakika ya 13, mfungaji Deus Kaseke na Mohamed Juma Mtwanga akawasawazishia Clove dakika ya 24.
Fundi;Stephen Bengo akienda chini na mpira wake baada ya kuchezewa rafu na Hamisi Ally wa KMKM |
Bado wamo; Bengo akiambaa na mpira pembeni ya mchezaji wa KMKM |
Mchezo wa pili wa Kundi B kati ya Simba SC na AFC Leopard ya Kenya utafuatia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Amaan.
Katika mchezo huo mchezaji wa timu ya KMKM Khamis Ali alipewa zawadi ya King’amuzi cha Azam TV na dishi lake kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika nyasi bandia za uwanja wa Amaan.
Wakati huo huo: Msemaji wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi, Farouk Karim amesema kwamba kufuatia kujitoa kwa Yanga SC, timu ya Ashanti United ya Ilala imechukua nafasi hiyo.
Farouk amesema Ashanti itawasili hapa kesho na usiku itamenyana na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, ambao utatanguliwa na mechi kati ya Azam FC na Spice Stars Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment