MRENO Cristiano Ronaldo amemtambia kwa mara nyingine, Msweden Zlatan Ibrahimovic, baada ya Real Madrid kuifunga bao 1-0 PSG katika mchezo wa kirafiki wa majira ya baridi mjini Doha.
Jese alifunga bao hilo pekee dakika ya19 na kumfanya Ronaldo aliyemnyanyasa Ibra katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka jana akiiwezesha Ureno kushinda mechi zote dhidi ya Sweden nyumbani na ugenini, aendeleze ubabe wake kwa mwenzake.
Mshambuliaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 20, ambaye amebukia kwenye timu ya vijana ya vigogo hao wa Hispania, hadi sasa amecheza mechi 16 na kuifungia mabao mawili timu hiyo.
Kifaa: Jese (wa pili kushoto na chini) akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi
Ibrahimovic alitaniana na kocha Carlo Ancelotti wakati wa mapumziko
Ibrahimovic na Ronaldo (chini) walikuwa nyota wa mchezo leo
Ibra akiruka kumzidi Ronaldo kupiga mpira kichwa katika mchezo wa kirafiki Doha
Ronaldo akipiga shuti
Ronaldo akiwatoka mabeki wa PSG
0 comments:
Post a Comment