NYOTA wa Bayern Munich, Franck Ribery ameuponda mfumo wa upigaji kura za kuchagua Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or na kusema alistahili zaidi kushinda tuzo hiyo kuliko Cristiano Ronaldo, kwa sababu alishinda mataji matano mwaka 2013, wakati mpinzani wake wa Real Madrid hakushinda chochote.
Mfaransa huyo alikubali kushika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi, Ronaldo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili katika sherehe za tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi Jumatatu iliyopita na pia amesema tuzo binafsi si muhimu kwake.
Ribery
alitwaa mataji ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya UEFA na Klabu Bingwa ya Dunia akiwa na Bayern mwaka 2013.Nyota huyo wa Ufaransa pia alisema kwamba yalifanyika mabadiliko katika mfumo wa upigaji kura mwaka huu kumsaidia Ronaldo, kwa kuongeza muda wa kupiga kura wakati nyota huyo wa Ureno alikuwa kwenye mazingira ya kuiwezesha nchi yake kuitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya Kombe la Dunia.
Hasira zake hazikuishia kwenye tuzo hiyo tu, bali pia uteuzi wa kikosi bora cha wachezaji 11 wa FIFA wa mwaka- kuhusisha wachezaji watatu tu wa Bundesliga,
licha ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2013 kuzikutanisha Bayern na
Borussia Dortmund.
Mfaransa huyo alikubali kushika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi, Ronaldo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili katika sherehe za tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi Jumatatu iliyopita na pia amesema tuzo binafsi si muhimu kwake.
0 comments:
Post a Comment