// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OKWI MARUFUKU KUCHEZA YANGA HADI KESI YAKE YA FIFA NA ETOILE IPATIWE UFUMBUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OKWI MARUFUKU KUCHEZA YANGA HADI KESI YAKE YA FIFA NA ETOILE IPATIWE UFUMBUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, January 22, 2014

    OKWI MARUFUKU KUCHEZA YANGA HADI KESI YAKE YA FIFA NA ETOILE IPATIWE UFUMBUZI

    Na Boniface Wambura, Ilala
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa la (FIFA).
    Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
    
    Imekuwaje tena mkubwa? Okwi akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa ya Yanga, Seif Ahmed 'Magari' kushoto
    Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
    Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
    Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
    Wakati huo huo: TFF imesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.
    Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
    Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI MARUFUKU KUCHEZA YANGA HADI KESI YAKE YA FIFA NA ETOILE IPATIWE UFUMBUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top