• HABARI MPYA

        Monday, January 27, 2014

        MOYES ATAKA AKINA MATA WENGINE WAWILI MAN UNITED

        BAADA ya kumsajili Juan Mata, kocha wa Manchester United, David Moyes amesema kwamba huo ni mwanzo, mengi mazuri yanakuja na ameweka bayana mpango wa kusajili nyota wengine wawili.
        "Huu ni mwanzo wa mengi yanayokuja. Nasonga mbele, Juan akiwa mwanzo wa harakati zangu,"alisema.
        Wasaka vipaji wa United waliwaangalia wachezaji Filipe Luis na Diego Costa wakiisaidia Atletico Madrid kushinda 4-2 dhidi ya Rayo Vallecano jana.
        Juan Mata anatarajiwa kuanza kuichezea United katika mechi dhidi ya Cardiff City kesho baada ya kusajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea.

        Quality: Moyes hopes Mata finds the form that made him Chelsea's player of the season two years in a row
        Kiwango: Moyes anatumai Mata atakuwa mwanzo wa kupata nyota wengine kuongeza nguvu kikosini mwake
        Atletico Madrid striker Diego Costa
        Atletico Madrid defender Filipe Luis
        Wanawindwa: Diego Costa (kulia) na Felipe Luis (kushoto) wapo kwenye rada za United
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MOYES ATAKA AKINA MATA WENGINE WAWILI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry