// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKWASA NA PONDA WAANZA KAZI YANGA, OKWI NA KIIZA WAAHIDI KUTUA DAR KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKWASA NA PONDA WAANZA KAZI YANGA, OKWI NA KIIZA WAAHIDI KUTUA DAR KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 03, 2014

    MKWASA NA PONDA WAANZA KAZI YANGA, OKWI NA KIIZA WAAHIDI KUTUA DAR KESHO

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MAKOCHA wapya wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa na Juma Nassor Pondamali leo asubuhi wameiongoza mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza, Uwanja wa Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam.
    Wachezaji hao wa zamani wa Yanga, walitangazwa rasmi na klabu hiyo kuajiriwa jana kupitia tovuti ya klabu, kufuatia uongozi kuvunja benchi zima la Ufundi, chini ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts na Wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mkenya Razack Ssiwa aliyekuwa kocha wa makipa.
    Labda kesho; Emmanuel Okwi ameahidi kutua Dar es Salaam kesho

    Mkwasa maarufu kama Master, amechukua nafasi ya Minziro aliyekuwa kocha Msaidizi na Pondamali ‘Mensah’ amechukua nafasi ya Ssiwa wakati uongozi bado upo kwenye mchakato wa kumpata mrithi wa Brandts.
    Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa klabu ya Yanga SC, Baraka Kizuguto amesema kwamba washambuliaji wawili Waganda wa timu hiyo, Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza sasa wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho.
    Kizuguto amesema amezungumza na wachezaji hao leo na wamemuambia walikwama kuwasili awali kama walivyotakiwa kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini wamemuhakikishia kesho watakuwa Dar es Salaam. 
    Kizuguto alisema baada ya kuwasili kesho, wachezaji hao wataanza mazoezi Jumatatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA NA PONDA WAANZA KAZI YANGA, OKWI NA KIIZA WAAHIDI KUTUA DAR KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top