MPIGA
tumba namba moja katika muziki wa dansi hapa nchini Soud Mohamed MCD
wa Twanga Pepeta amefariki dunia usiku huu mjini Moshi.
MCD alikuwa huko kwa zaidi ya miezi miwili akiugua na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri lakini hali ikabadilika usiku huu na kuaga dunia.
Msemaji wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani ameithibitishia Saluti5 kuwa MCD amefarikidunia.
Wiki
iliyopita MCD aliongeana Saluti5
na kusema anaendelea vizuri na kwamba ile hatua ngumu ya dozi kali
ya kifua kikuu alikuwa ameshaivuka na sasa amebadilishiwa dawa.
MCD
aliongea kwa matumaini makubwa kuwa atarejea jukwaani muda si mrefu.
Majuzi
MCD aliomba nauli yakurejea Dar kwa uongozi wa Aset,
jambo ambalo lilitekelezwa haraka na pengine kama siku zake za kuishi duniani zilikuwa bado zipo japo kwa
wiki moja mbele, MCD angeaga dunia akiwa Dar es Salaam.
Katika uhai
wake bendi zingine alizozitumikia MCD ni na Diamond Sound, Mashujaa Band.
MCD
AMEFIA MLANGO WA HOSPITALI YA KCMC…
KWA
mujibu wa mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka, mpiga tumba wa
Twanga Pepeta, Soud
Mohamed “MCD” aliyefariki Jumatatu (jana) usiku,
mauti yalimfika mara tu baada ya kufika kwenye mlangowa hospitali ya KCMC Moshi.
Akiongea na
Saluti5 muda mfupi baada ya taarifa za msiba, Asha Baraka alisema hadi mchana wa leo
(Jumatatu) MCD alikuwa kwenye hali nzuri, lakini baadaye hali ikaanza kubadilika.
Asha
Baraka anasema dada wa marehemu amemjulisha kuwa ilipofika usiku MCD
aliendelea kujiskia ovyo na wakaamua kumkimbiza hospitali ya KCMC.
Lakini kwa mujibu wa maelezoya
dada huyokupitiakwaAsha Baraka, MCD alifarikimaratuwaliofikakwenyemlangowahospitalihiyo.
Mwiliwa
MCD umehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
MCD
alikuwa Moshi ambako ndiko nyumbani kwao alikozaliwa kwa ajili ya kujiuguza maradhi ya kifua kikuu.
0 comments:
Post a Comment