KOCHA David Moyes amesema kwamba hakuna uhakika kama Wayne Rooney atasaini Mkataba mpya Old Trafford ikiwa Manchester United itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Rooney, ambaye ataukosa mchezo wa leo wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA dhidi ya Swansea kutokana na maumivu nyonga, atafikia tamati ya Mkataba wake wa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki mwishoni mwa msimu.
United iko tayari kuanza mazungumzo na Rooney juu ya mkataba mpya, lakini inasadikiwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kusubiri hadi baada ya Fainali za Kombe la Dunia kabla ya kuamua mustakabali wake.
Anaondoka? Wayne Rooney, bado hajasaini mkataba mpya Man United, hali inayozua hofu juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo
Matumaini ya United kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England yalipata pigo lingine katika siku ya mwaka mpya iliposukumiwa hadi nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani na Tottenham.
Inaibua hofu kwamba Rooney, aliyetakiwa kwa dau la Pauni Milioni 30 na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita, anaweza kuondoka United iwapo haitafuzu Ligi ya Mabingwa.
Moyes amesema jana kwwamba: "Tutalazimika kubiri ili kuona nini kitatokea katika mazingira haya,". Alipoulizwa kama mshambuliaji huyo wa England ana furaha United, Moyes alisemas: "Nafikiri ikiwa utaangalia anavyocheza, dhahiri anacheza katika kiwango chake bora,".
0 comments:
Post a Comment