Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Zdravko Logarusic anatarajiwa kuwasili alfajiri ya kesho, akitokea kwao Croatia alipokuwa kwa mapumziko ya mwaka mpya, imeelezwa.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Swedi Nkwabi ameiambia BIN ZUBEIRY leo mjini hapa kwamba, Logarusic atawasili majira ya Saa 9:50 usiku na mchana wa kesho atapanda boti kuja Zanzibar kuungana na timu.
Nkwabi alisema utaratibu mzima wa kumpokea mwaimu huyo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kumsafirisha kuja Zanzibar umekwishaandaliwa.
Simba SC leo itacheza mechi ya pili ya Kundi B, Kombe la Mapinduzi bila Logarusic, ikiongozwa na kocha wake Msaidizi, Suleiman Matola ‘Veron’, ikimenyana na KCC ya Uganda, Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 2:00 Usiku.
Matola aliiongoza vyema Simba SC katika mchezo wake wa kwanza ikailaza bao 1-0 AFC Leopard ya Kenya juzi mjini hapa, ambalo lilitiwa kimiani na Amri Ramadhani Kiemba, baada ya kazi nzuri ya Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’.
Mchezo wa kati ya Simba SC na KCC, utatanguliwa na mechi nyingine ya Kundi B, baina ya wenyeji KMKM na Leopard utakaoanza Saa 10:00 Uwanja wa Amaan pia.

Kesho atakuwa Zanzibar; Kocha wa Simba SC, Zdravko Logarusic kesho atakuwa Zanzibar |
Nkwabi alisema utaratibu mzima wa kumpokea mwaimu huyo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kumsafirisha kuja Zanzibar umekwishaandaliwa.
Simba SC leo itacheza mechi ya pili ya Kundi B, Kombe la Mapinduzi bila Logarusic, ikiongozwa na kocha wake Msaidizi, Suleiman Matola ‘Veron’, ikimenyana na KCC ya Uganda, Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 2:00 Usiku.
Matola aliiongoza vyema Simba SC katika mchezo wake wa kwanza ikailaza bao 1-0 AFC Leopard ya Kenya juzi mjini hapa, ambalo lilitiwa kimiani na Amri Ramadhani Kiemba, baada ya kazi nzuri ya Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’.
Mchezo wa kati ya Simba SC na KCC, utatanguliwa na mechi nyingine ya Kundi B, baina ya wenyeji KMKM na Leopard utakaoanza Saa 10:00 Uwanja wa Amaan pia.
0 comments:
Post a Comment