RATIBA ya michuano ya Afrika mwaka huu imekwishatoka na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, watafungua dimba nyumbani na Komorozine ya Comoro katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC wataanzia nyumbani pia na Azam Ferroviario Da Beira ya Msumbiji katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, wakati marudiano yatakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February 2014.
Azam mwakani watacheza kwa mara ya pili michuano ya Afrika, wakati Yanga SC ilicheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo mwaka 1969.
Miaka ya karibuni matokeo ya klabu za Tanzania yamekuwa si ya kuridhisha na tulishuhudia mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa, Simba SC na Yanga zikishindwa japo kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Ukitazama rekodi ya klabu za Tanzania kwenye michuano ya Afrika, Simba ndiyo klabu yenye rekodi nzuri zaidi katika michuano hiyo, ikiwa imewahi kufika Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003, wakiwatoa wapinzani wa Yanga mwaka huu, Zamalek na pia wakati michuano hiyo ikiitwa Klabu Bingwa Afrika walicheza Nusu Fainali mwaka 1974.
Yanga wanafuatia rekodi hiyo ya watani wao wa jadi, wakiwa wamecheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa 1998, na wakati michuano hiyo ikiitwa Klabu Bingwa Afrika, walicheza Robo Fainali mara mbili 1969 na 1970 na walifika pia Robo Fainali ya Kombe la Washindi mwaka 1996.
Ukitazama ratiba ya mwaka huu, hakuna ubishi kwamba Yanga na Azam wamepangiwa timu za kawaida tu kwa viwango vyao, ambazo kama watakuwa na maandalizi mazuri watavuka mtihani huo.
Lakini pamoja na ukweli huo, Yanga na Azam hawatakiwi kuwadharau wapinzani wao. Wanatakiwa kufanya maandalizi mazuri, ili wawatoe kwa uhakika.
Angalau Azam wamekwishaanza maandalizi hivi sasa na wako ziarani Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini Yanga hata kocha Mkuu hadi sasa hawana tangu wavunje benchi lao la ufundi.
Yanga baada ya kufungwa 3-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba SC Desemba 21 katika mechi ya Nani Mtani Jembe wakafukuza benchi zima la Ufundi chini ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts na Wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Razack Ssiwa.
Baada ya hapo, ni juzi wamewaajiri wachezaji wao wa zamani, Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha Msaidizi na Juma Pondamali kuwa kocha wa makipa, wakati bado wapo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya Mkuu.
Labda ni kwa sababu ya mabadiliko ya benchi la ufundi waliyofanya- lakini ipo haja ya uongozi wa klabu hiyo kufanya kila kinachowezekana kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa kambini mapema na kujiandaa vema.
Nasema kujiandaa vema, kwa sababu wachezaji wanatakiwa kujengwa kikamilifu kuanzia katika nguvu, stamina, pumzi na uwezo wa kuuchezea mpira- hivi vitu haviwezekani ndani ya wiki mbili.
Maana yake imekuwa kawaida ya timu zetu kukurupuka na kuja kuanza maandalizi wiki mbili kabla ya mashindano, matokeo yake zikitolewa visingizio vinakuwa kibao. Watu wamekwishachoka na visingizio na sasa wanataka matokeo mazuri na ndiyo maana mpendwa wenu, BIN ZUBEIRY nimeona huu ni wakati mwafaka kukumbushana umuhimu wa maandalizi. Wasalaam.

0 comments:
Post a Comment