KINDA Adnan Januzaj amempiku mchezaji mwenzake, Ashley Young na kushika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji wanaoongoza kupewa kadi za njano kwa kujirusha wakidanganya wamechezewa rafu kwenye historia ya Ligi Kuu ya England.
Winga huyo wa Manchester United, alipewa kadi ya tano ya njano msimu huu katika mechi dhidi ya Tottenham siku ya mwaka mpya na refa Howard Webb baada ya kujirusha alipokabiliana na Danny Rose.
Januzaj, ambaye amepewa kadi tatu za njano kwa kwenda chini kiulaini, sasa yupo nyuma ya Gareth Bale katika historia ya magwiji wa kujirusha, licha ya kucheza mechi 14 tu.
Kadi: Adnan Januzaj akionyeshwa kadi ya njano na referee Howard Webb, Manchester United ikifungwa 2-1 na Tottenham jana
Ameenda chini: Januzaj akianguka chini baada ya kukabiliana na beki wa Spurs, Danny Rose kipindi cha pili
Januzaj, akipambana na beki wa Tottenham, Kyle Walker alishindwa kuisaidia timu yake kuepuka kipigo cha timu ya Tim Sherwood
Kitendo cha kujirusha adhabu yake ni kadi tu katika jitihada za FA kupambana na desturi hiyo mbaya, sheria ambayo ilianzishwa mwaka 2008 ili kuhakikisha tatizo hilo haliwi sugu katika soka ya England.
Bale, ambaye aliondoka England na kuhamia Hispania kwa dau la rekodi ya dunia akijiunga na Real Madrid msimu uliopita, aliweka rekodi ya pekee ya kujiangusha akiwa Tottenham, baada ya kupewa jumla ya kadi saba za njano enzi zake akiichezea klabu hiyo ya London Kaskazini.
Lakini Januzaj kupewa kadi tatu za njano ndani ya mechi 14 tu, nane kati ya hizo akainza tangu mwanzo- awe mchezaji wa kuchungwa mno na mabeki wa Ligi Kuu dhidi ya janja yake hiyo.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye anachezea kwa msimu wake wa kwanza kikosi cha kwanza cha United, awali alipewa kadi kwa kujirusha katika mechi dhidi ya Sunderland na West Ham kabla ya tukio la Jumatano Uwanja wa Old Trafford.
Kinda huyo sasa analingana na mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres katika orodha ya 'wataalamu wa kujirusha', huku wachezaji wengi wakiwa wamepewa kadi mbili mbili, wakiwemo Young, washambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez, West Ham, Andy Carroll, Man United, Javier Hernandez na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Mario Balotelli.
Hakuna rafu: Januzaj alipewa kadi ya njano baada ya kujiangusha karibu na mchezaji wa West Ham, James Collins siku Manchester United ikishinda 3-1 Desemba mwaka jana
Januzaj alifunga mabao mawili lakini akapewa kadi ya njano na refa Chris Foy kwa kujirusha dhidi ya Sunderland Uwanja wa Light
Jose Mourinho anaamini Luis Suarez alistahili kadi ya njano kwa kujirusha Liverpool ilipomenyana na Chelsea mwishoni mwa wiki iliyopita
Kiungo wa Everton, Ross Barkey (kushoto) alipewa kadi ya njano kwa kujirusha dhidi ya mahasimu wao, Liverpool
Kiungo wa Chelsea, Oscar alipewa kadi ya njano kwa kujaribu kusaka penalti dhidi ya Southampton
Winga wa zamani wa Tottenham, Gareth Bale (kushoto) akipewa kadi ya njano kwa kujirusha, hivyo kuongoza katika msimamo wa orodha ya wachezaji magwiji wa kujirusah tangu Agosti mwaka 2008 katika Ligi Kuu England
0 comments:
Post a Comment