Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akizungumza na Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo, Mganda Moses Basena aliyeipa kamera mgongo jana wakati timu hiyo ikimenyana na Chuoni ya Unguja katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Kushoto ambao wanasikilizia 'kama hawafuatilii' ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Ibrahim Masoud 'Maestro' na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu yo, Geoffrey Nyange 'Kaburu' ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
 |
Tazama Hans Poppe anavyomuangalia Basena na wageukie Mestro na Kaburu wanavyosikilizia. Kuna usalama kweli hapa?
 |
Kulia ni Mjumbe mwingine wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Pamba akimuangalia Hans Poppe 'anavyomuwakia' Basena
|
|
|
0 comments:
Post a Comment