MCAMEROON Samuel Eto'o amelichangamsha Jiji la London leo baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa 3-1 wa Chelsea dhidi ya Manchester United, Uwanja wa Stamford Bridge.
Eto'o alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza dakika ya 17 na 45 na baadaye dakika ya nne tangu kuanza kipindi cha pili akakamilisha hattrick yake kabla ya kumpisha Fernando Torres dakika ya 79.
Javier Hernandez 'Chicharito' aliyetokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Ashley Young aliwafungia Mashetani Wekundu bao la kufutia machozi dakika ya 78.
Nemanja Vidic alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei na Man United ikaishiwa nguvu kabisa.
Ushindi huo, unaifanya The Blues ya Jose Mourinho ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 22, ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City pointi 50 na Arsenal pointi 51, wakati United ya David Moyes inabaki nafasi ya saba pointi 37.
Katika mchezo uliotangulia, Tittenham Hotspur imeifunga Swansea City mabao 3-1 nyumbani kwake. Mabao ya Spurs yalifungwa na Emmanuel Adebayor dakika ya 35 na 71 na Chico aliyejifunga dakika 53, wakati la wenyeji la kufutia machozi lilifungwa na Bony dakika ya 78.

0 comments:
Post a Comment