SHIRIKISHO la Soka
Afrika (CAF) leo limeupa kibali cha Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,Dar
es Salaam unaomilikiwa na klabu ya Azam Fc kutumika kwa michuano ya klabu
barani Afrika .
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa Naibu
Mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo, Khaled Nassar, Uwanja wa Azam
Compex umekidhi vigezo vyote
vinavyohitajika na CAF kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa.
Moja ya majukwaa ya Azam Complex |
Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda
TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguzi wake kutoka Zimbabwe, Wilfried Mukuna
kuja kukagua Uwanja huu na akawasilisha ripoti CAF, ambayo imefanya shirikisho
hilo litoe kibali hicho.
Uongozi wa Azam FC umemshukuru Mukuna, TFF chini ya Rais wake,
Jamal Malinzi na uongozi wa CAF, yenye makao yake makuu Cairo, Misri hasusan
Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa uwazi na weledi wa hali ya
juu.
Azam FC pia inawataarifu wapenzi wake kwamba kuanzia msimu
huu mechi zake za Kombe la Shirikisho zitafanyika Uwanja huo. Azam itaanza na
Ferroviarrio ya Msumbiji mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment