BAO la Adam Lallana limeosha kuipa sare ya 2-2 Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya vinara, Arsenal ambao sasa wanawafungulia milango Manchester City na Chelsea kwenye mbio za ubingwa.
Nyota huyo wa kimataifa wa England alifunga kiasi cha dakika mbili baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal dakika ya 52 na kumuachia presha kocha Arsene Wenger katika kampeni za ubingwa.
Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Jose Fonte dakika ya 21, lakini Oliver Giroud akaisawazishia The Gunners dakika ya 48. Arsenal walimaliza mechi wakiwa 10 baada ya Mathieu Flamini kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Arsenal sasa inakuwa na pointi 52 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 50 na Chelsea pointi 49, ingawa zote zimecheza mechi 22.
La uchungu: Nyota wa Southampton, Adam Lallana, katikati, akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Arsenal
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, katikati, akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la pili
Mfaransa hatari: Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha
0 comments:
Post a Comment