Na Mahmoud Zubeiry, Jangwani
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji amesema kwamba wataboresha benchi la Ufundi la timu na habari zaidi kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba makocha wote wanaondolewa, kufuatia kipigo cha jana cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Manji hakuzungumzia kwa undani kuhusu benchi la Ufundi, zaidi ya kusema wataboresha, lakini habari za ndani zinasema Kocha Mkuu, Mholanzi Ernie Brandts na wasaidizi wake wote, mzalendo Freddy Felix Minziro na Mkenya Razack Ssiwa wanaondolewa.
Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina amesema kwamba, makocha wote wameonyesha hawafai na wanaondolewa ili kuinusuru timu.
Wanaondoka: Kocha wa Yanga, Ernie Brandts anaweza kuondolewa pamoja na wasaidizi wake baada ya kipigo cha SImba cha 3-1 jana Uwanja wa Taifa
REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA
Yanga 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
Yanga 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Yanga 3-1 Toto African (Ligi Kuu)
Yanga 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
Yanga 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu)
Yanga 2-0 Azam FC (Ligi Kuu)
Yanga 2-0 Coastal (Ligi Kuu)
Yanga 0-1 Tusker (Kirafiki)
Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (Kirafiki)
Yanga SC 0-2 Emmen FC (Kirafiki)
Yanga SC 1-2 Denizlispor FC (Kirafiki)
Yanga SC 3-2 Black Leopard (Kirafiki)
Yanga SC 2-1 Black Leopard (Kirafiki)
Yanga SC 3-1 Prisons (Ligi Kuu)
Yanga 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Yanga 4-0 African Lyon (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-0 Azam FC (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-0 Toto Africans (Ligi Kuu)
Yanga 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Yanga SC 0-0 Polisi (Ligi Kuu)
Yanga SC 3-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-1 JKT Mgambo (Ligi Kuu)
Yanga SC 3-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu) alikuwa mgonjwa hakuja Taifa.
Yanga SC 1-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu)
Yanga 1-1 Express (Kiarfiki, Mwanza)
Yanga 1-2 Express (Kiarfiki, Shinyanga)
Yanga 0-0 Rhino FC (Kiarfiki, Tabora)
Yanga 2-2 URA (Kirafiki Taifa)
Yanga 3-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki Taifa)
Yanga 1-0 2Pillars (Nigeria, Kirafiki Dar)
Yanga 4-1 SC Villa (Kirafiki, Taifa)
Yanga SC 1-0 Azam (Ngao)
Yanga 5-1 Ashanti (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-1 Coastal U (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu)
Yanga 2-3 Azam FC (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Yanga 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Yanga 3-3 Simba SC (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu)
Yanga 4-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Yanga 3-2 KMKM (Kiarafiki)
Yanga 1-3 Simba SC (Mtani Jembe)
Manji amesema anasafiri nje ya nchi kwa mapumziko ya kuukaribisha mwaka mpya na Makamu wake, Clement Sanga ndiye atakaimu nafasi yake.
Na Manji amesema juu ya hatua nyingine zilizochukuliwa, Sanga ndiye atakayezungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni na kwamba hayo tayari ni maamuzi ya Kamati ya Utendaji.
Hadi hivi sasa, Brandts aliyeingia Yanga Oktoba mwaka jana akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet amekwishaiongoza timu hiyo katika mechi 50, akiiwezesha kushinda mechi 29, sare 13 na kufungwa nane.
Brandts ameipa Yanga SC taji moja la ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita na msimu huu hadi sasa ameifanya timu hiyo iongoze Ligi Kuu baada ya mzunguko wa kwanza.
Katika Mkutano wake wa leo asubuhi makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Manji amemtetea kipa Juma Kaseja aliyesimama langoni jana katika mechi ya Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Yanga ikilala 3-1.
Akimjibu Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali aliyeushutumu uongozi kusajili Juma Kaseja ni makosa, Mwenyekiti huyo alisema hawakumsajili kipa huyo kwa ajili ya kuifunga Simba SC.
“Huyu mzee nadhani umri umemzidi, lakini nataka nimkumbushe, huyo Ivo Mapunda aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongzi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi na Simba SC,”.
“Lakini pia nataka nimuulize, wakati Simba inarudisha mabao yote matatu Kaseja alikuwapo langoni? Nadhani hivi vitu si vizuri, tuache kulaumiana tushikamane kwa mustakabali mzuri wa timu,”alisema Manji.
Manji amesema wanaheshimu uwezo wa Kaseja kwa sababu ndiye kipa aliyedaka mechi nyingi za mashindano ya Afrika kati ya makipa wote nchini, hivyo thamani yake haitashuka kwa kufungwa mabao matatu jana.
Pamoja na hayo, Manji amesema kwamba mechi ya jana haikuwa na uzito wowote kwao ni sawa na bonanza au fete, hivyo kufungwa haijawaumiza.
“Tuliamua kucheza kumfurahisha mdhamini TBL, tumefungwa lakini bado tunaongoza ligi, hatujapoteza pointi hata moja, ile ilikuwa fete tu,”alisema Manji.
Manji amekiri Simba SC walicheza vizuri zaidi jana na walistahili ushindi na anawapongeza kwa hilo, pamoja na wadhamini, TBL kwa kuandaa mechi hiyo.
Manji amesema kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika wataboresha timu na benchi la ufundi na timu itaenda tena kambini Ulaya, hivyo anaamini mwakani makali yao yatafufuka na watatetea ubingwa.
0 comments:
Post a Comment