// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC KUANZA NA VIBONDE WA COMORO LIGI YA MABINGWA, AZAM FC NA FERROVIARIO KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC KUANZA NA VIBONDE WA COMORO LIGI YA MABINGWA, AZAM FC NA FERROVIARIO KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 16, 2013

    YANGA SC KUANZA NA VIBONDE WA COMORO LIGI YA MABINGWA, AZAM FC NA FERROVIARIO KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC, watafungua dimba nyumbani na Komorozine ya Comoro katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC wataanzia nyumbani pia na Azam Ferroviario Da Beira ya Msumbiji katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho.
    Yanga wataanza na vibonde wa Comoro Ligi ya Mabingwa Afrika

    Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, wakati marudiano yatakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February 2014. 
    Azam na Ferroviarrio

    Kwa mujibu wa droo iliyopangwa leo mjini Marrakech, Morocco, klabu 52 zitamenyana katika Raundi ya Awali ya michuano ya 18 ya Ligi ya Mabingwa mwakani kusaka nafasi za kuungana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, Coton Sport ya Cameroon, TP Mazembe ya DRC, Hilal ya Sudan, CS Sfaxien na Esperance Sportive za Tunisia katika Raundi ya Kwanza.
    Wawakilishi wa Zanzibar katika Shirikisho, Chuoni wataanzia nyumbani na How Mine ya Zimbabwe, wakati katika Ligi ya Mabingwa KMKM wataanzia ugenini na Dedebit ya Ethiopia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC KUANZA NA VIBONDE WA COMORO LIGI YA MABINGWA, AZAM FC NA FERROVIARIO KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top