KLABU ya Manchester United inahofia jitihada zake za beki mpya wa kushoto katika usajili wa dirisha dogo Januari hauwezi kuvunja matunda, kwa Everton na Southampton kutokuwa na mpango wa kuwaachia wachezaji wake Leighton Baines na Luke Shaw.
Kocha wa United, David Moyes alijaribu bila mafanikio kutaka kumsaini Baines kutoka klabu yake ya zamani mapema msimu huu, baada ya Patrice Evra kusema anahitaji ushindani wa maana wa namba katika nafasi yake.
Lakini juhudi za United zimezimwa na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright na pamoja na hayo Moyes ameambiwa na Mtendaji Mkuu wa klabu yake, Ed Woodward kwamba hana fedha za kutoa kwa ajili ya usajili wa mwezi ujao.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanahofia watakutana na mazingira yale yale kutoka klabu ya Merseyside, pamoja na Southampton juu ya Shaw wanayemtaka.
Anaowatolea macho: David Moyes anamtaka Baines na beki wa Southampton, Luke Shaw, lakini kuna hatari akawakosa
Shaw, mwenye umri wa miaka 18, pia yupo kwenye rada za Chelsea, lakini Southampton imeweka wazi kwamba haimuuzi mchezaji huyo.
United inahaha kusaka beki wa kushoto kutokana pia na Mholanzi, Alexander Buttner kushindwa kufanya vizuri tangu asajiliwe na Sir Alex Ferguson mwaka 2012.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, binafsi anatakiwa na Tottenham katika usajili huu wa Januari, ameanza katika mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu msimu huu, maana yake kwamba Evra, akiwa na umri wa miaka 32, amebeba majukumu makubwa ya timu katika nafasi hiyo.
Tayari msimu huu, beki huyo wa Ufaransa amecheza mechi 29 za klabu yake na hi yake katika mashindano yote.
Majukumu mazito: Akiwa hana msaidizi wa maana, Patrice Evra amecheza mechi nyingi beki ya kushoto msimu huu
0 comments:
Post a Comment