MABAO mawili ya Wayne Rooney leo yameinusuru Manchester United kulala mbele ya kikosi cha Andre Villas-Boas, Tottenham baada ya kupata sare ya 2-2 Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Kyle Walker alifunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 18, lakini beki huyo wa kulia wa England akamsetia Rooney kuisawazishia Manchester United dakika ya 32.
Villas-Boas alikaribia kupata ushindi baada ya Sandro kufunga bao la pili umbali wa mita 25 akimtungua kipa David De Gea dakika ya 54, lakini Rooney akasawazisha tena kwa penalti dakika ya 57.
Kikosi cha Tottenham kilikuwa: Lloris, Walker, Dawson, Chiriches, Vertonghen, Sandro, Paulinho, Lennon/Townsend dk65, Dembele, Chadli/Sigurdsson dk84 na Soldado/Defoe dk71.
Man United: De Gea, Smalling, Vidic, Evans, Evra, Cleverley, Jones, Valencia/Nani dk83, Kagawa/Young dk83, Welbeck/Hernandez dk72 na Rooney.
Mkombozi: Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney akiisawazishia timu yake kwa penalti dhidi ya Spurs
Rooney akisngilia baada ya kuifungia United
Sandro akishangilia baada ya kuifungia Tottenham
0 comments:
Post a Comment