NYOTA wa Barcelona, Mbrazil Neymar jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal na kupaa kileleni mwa La Liga kwa pointi tano zaidi dhidi ya wapinzani wao, Real Madrid.
Wakati Messi akiwa bado majeruhi, huku Xavi akipumzishwa benchi, kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song na Cesc Fabregas walicheza kwa pamoja katika safu ya kiungo.
Barcelona ilitawala na mchezo mwanzoni na alikuwa ni Neymar aliyeanza kufunga dakika ya 28, Mbrazil huyo akiwa mchezaji wa tano tofauti kuifungia klabu hiyo kwa penalti msimu huu, baada ya Mario Gaspar kuunawa mpira katika harakati za kuokoa krosi ya Jordi Alba.
Villarreal ilisawazisha bao hilo dakika nne tangu kuanza kipindi cha pili, wakati Mateo Musacchio alipounganisha kwa kichwa kona. Baada ya kuwaruhusu Villrreal kuchomoa bao hilo, kocha wa Barca, Tata Martino alimuingiza Xavi kuchukua nafasi ya Alex Song.
Fabregas alivunja mtego wa kuotea uliowekwa na wapinzani wao kwa pasi ambayo Alexis Sanchez aliirudisha kwa Neymar aliyefunga bao lake la 10 msimu huu katika mashindano yote.
Katika mechi nyingi za La Liga jana, Real Madrid ililaimishwa sare ya 2-2 na Osasuna ugenini Uwanja wa El Sadar, Pamplona. Mabao yote ya wenyeji yalifungwa na Oriol Riera dakika ya 16 pasi ya Marc Bertran na dakika ya 39, wakati ya Real yalifungwa na Isco dakika ya 45 pasi ya Cristiano Ronaldo na Pepe daki ya 80 pasi ya Isco.
Malaga imeifunga 1-0 Getafe, Rayo Vallecano imefungwa 2-0 na Granada CF, Levante imeifunga 2 - 1 Elche.

Neymar ameendelea kuibeba Barcelona wakati ambao Messi ni majeruhi |

Alitoka kapa;Ronaldo jana hakufunga Real ikitoa sare ya 2-2 La Liga |
Katika mechi nyingi za La Liga jana, Real Madrid ililaimishwa sare ya 2-2 na Osasuna ugenini Uwanja wa El Sadar, Pamplona. Mabao yote ya wenyeji yalifungwa na Oriol Riera dakika ya 16 pasi ya Marc Bertran na dakika ya 39, wakati ya Real yalifungwa na Isco dakika ya 45 pasi ya Cristiano Ronaldo na Pepe daki ya 80 pasi ya Isco.
Malaga imeifunga 1-0 Getafe, Rayo Vallecano imefungwa 2-0 na Granada CF, Levante imeifunga 2 - 1 Elche.
0 comments:
Post a Comment