KOCHA Jose Mourinho na Brendan Rodgers waliingia kwenye vita ya maneno jana baada ya mechi, ambayo Chelsea iliifunga Liverpool 2-1 katika Ligi Kuu y England.
Samuel Eto’o alifunga bao la ushindi Uwanja wa Stamford Bridge, aikitumia makosa ya Simon Mignolet.
Lakini kocha wa Chelsea, Mourinho baadaye akamuita mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez mcheza sarakasi za kujirusha, kufuatia nyota huyo wa Uruguay kulalamika mara mbili kunyimwa penalti na refa Howard Webb baada ya kudhibitiwa kwenye eneo la hatari.
Utata: Mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez katika eneo la penalti
Amemgusa: Mguu wa kulia wa Eto'o unaonekana ukimzuia Suarez asimfikie Cesar Azpilicueta anayekimbia na mpira
Suarez akiugulia maumivu huku akienda chini katika eneo la penalti la Chelsea kipindi cha jana
Penalti jamani: Suarez akililia penalti, lakini refa Howard Webb alimpuuza
Mourinho alisema: "Hii ni nchi maalum. Mimi si Muingereza, lakini nahisi nina majukumu ya kutetea thamani fulani ya soka hii.
"Moja kati ya vitu vizuri tulivyonavyo ni hatupendi msisimko. Mazingira haya kwenye boksi, kwa Azpilicueta na Eto’o, yazuie au mpe kadi ya njano Suarez. Si nzuri kwa mchezo wetu.
Haijamvutia: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini Suarez alistahili kuonyeshwa kadi ya njano kwa udanganyifu jana Uwanja wa Stamford Bridge
Mourinho na Suarez walitaniana kidogo kabla ya kuanza kipindi cha pili jana
Sarakasi: Mourinho amemtuhumu Suarez kwa kucheza mchezo wa kujirusha kwenye bwawa la kuogelea baada ya timu yake kushinda 2-1
"Eto’o aliingia ndani na ilionekana kama mtu fulani kampiga (Suarez) nyuma. Kwangu, ile ni kadi ya njano ya dhahiri. Alifanya mchezo wa kujirusha kwenye bwawa la kuogelea kujaribu kutafuta penalti, kwa sababu ni mweledi sana anajua yuko kwenye eneo la penalti na mashabiki wa Liverpool wapo nyuma yake. Ikiwa mchezaji wa Chelsea angefanya hivyo, ningemuambia usifanye hivyo,".
Amekosa maneno: Refa Howard Webb akizungumza na Suarez, lakini hakumpa kadi ya njano nyota huyo wa Uruguayan
Anaenda chini: Suarez akienda chini baada ya kukabiliana na beki wa Chelsea, Gary Cahill
Rodgers, ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Mourinho, alijibu mapigo kwa kusema Eto’o alistahili kupewa kadi nyekundu kwa rafu aliyomchezea Jordan Henderson kwa sababu alimfuata na kumgonga mguuni, lakini hakupewa hata kadi ya njano.
Na akasema pia kitendo cha Eto’o kumzinia njia Suarez kilistahili penalti.
Heshima: Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers (kushoto) aliwahi kufanya kazi chini ya Mourinho awali
Rodgers anaamini mshambuliaji wa Chelsea, Eto'o alistahili kadi nyekundu kwa rafu mbaya aliyomchezea kiungo Jordan Henderon
Baada ya kunusurika katika rafu aliyomchezea Henderson, Eto'o akaenda kufunga bao la ushindi la Chelsea
0 comments:
Post a Comment